Ibadhi.com

AINA ZA NAJSI

Tambua  Ewe Mwanafunzi, Allah akurehemu kuwa najsi ziko za aina nyingi.

1. Kuna najsi zinazotoka katika moja kati ya tupu mbili, nazo ni kama: Manii, Madhii, Wadii, Damu ya hedhi, damu ya nifasi, maji-maji yanayotoka katika tupu ya mwanamke wakati wa kutoharika kwao, Choo kidogo (mkojo), Choo kikubwa (kinyesi).

2. Kuna najsi zinazotoka kupitia mdomoni, nazo ni kama vile: Matapishi na Macheuo.

3. Kuna najsi zinazotoka kupitia puani, nazo ni kama vile: Damu ya mwina.

4. Halkadhalika kuna najsi nyengine zisokuwa hizo, nazo ni kama vile: Unyevunyevu wa mzoga, damu inayochirizika, Nguruwe, Mbwa, Tumbiri, Vinyesi vya Wanyama wakali, na mikojo yao, na Mikojo ya wanyama wote kwa jumla.

TANBIHI MUHIMU SANA

Vinyesi vya wanyama wenye kwato kama vile: Farasi, Nyumbu, Punda, Ng'ombe, Mbuzi [1], n.k si NAJSI.

 -------------------------------------------------------------------------------------------------------
[1]- Amesema Al-Imaam Nuru-ddiin Assaalimiyy (r.t) katika kitabu chake Al-Ma'aarij juzuu (5/ sahifa ya 57): ((Wengi katika Maulamaa wetu wamewafikiana juu ya utohara wa vinyesi vya wanyama wenye kwato kama vile: Farasi, Nyumbu na Punda)).

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment