114:UGUMU WA MAISHA UNATOKANA NA NINI?

Written by

You have a new Question by:

Nurudn Saidi from

Tanzania

--------------------------------------

Swali:

Ugumu wa maisha unatokana na nini?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Ugumu wa maisha unatokana na kuacha mfumo wa maisha alouchagua Allah mtukufu kwa viumbe wake, na kufuata mifumo inayotokana na akili finyu za mwanadamu.

Mifumo ya kijamaa ukomunisti na ubepari ambayo imetungwa na wanadamu imeshindwa kumletea mwanadamu furaha aloitarajia.

Ukomunisti ni zao LA kushindwa kwa Ubepari, Ujamaa ni marekebisho ya Ukomunisti.
Ubepari ni zao LA kushindwa kwa Mafunzo ya kanisa katika karne ya 18 kuleta furaha kwa mwanadamu.

Kwa hiyo mifumo yote iliyotawala na inayotawala ulimwengu Leo hii imeshindwa na umebaki mfumo mmoja tu. Nao ni mfumo wa Allah mtukufu.

Mfumo huo sio katika baadhi ya mambo na kuacha mengine, Bali inatakiwa ufanyiwe kazi mfumo huo katika kila kitu ili uje na matunda yaliyotarajiwa.
Uislam ulivyokuwa umetamalaki uliweka mfano bora wa ubinadamu ambao haujawahi kutokea mpaka Leo.
Anasema Allah mtukufu:
(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)
Allah mtukufu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakafanya mema, atawatawalisha katika ardhi kama alivyowatawalisha waliopita kabla yao, na atawasimamishia dini yao [mfumo wa maisha] alouridhia kwao wao, na atawabadilishia khofu yao kuwa ni amani, wakiniabudu mimi hawanishirikishi na chochote, watakaokufuru baada ya hapo hao ndio waovu.
[Surat An-Nur 55]

Kwa hivyo inatakiwa ziwepo jitihada za Makusudi za kusimamisha dini ya Allah mtukufu katika ardhi, kisiasa, kiuchumi, kifikra, kitamduni, lugha, na mengineyo.

Hayo hayatimii ispokuwa ni kwa jamii kwanza kuwa na ilmu na yaqini juu ya uislam wao, wausimamshe katika nafsi na familia zao, kila mmoja awe ni Quran inayotembea, kila mmoja aone haja ya kuutaka uislam usimamie maisha yake na hata kama si wote lakini inatosha nusu ya waislamu kuwa na hisia hizo katika eneo miongoni mwa maeneo au nchi miongoni kwa nchi ili waweze kusimamisha uislam kama itakiwavyo.

Inapokuwa hakuna utayari huo kwa wengi, au utayari ukawepo bila ya ilmu ya kutosha inakuwa ni vurugu kama tunavyozishuhudia katika baadhi ya makundi.
Na hapo mambo huzidi ugumu na kuharibika kwa kuitumia dini katika Yale yasiyokubaliwa na dini kama kuuwa hovyo, n.k.

Tunamuomba Allah mtukufu atuandikie kuona uislam,waislam na mfumo wao ukisimamia furaha ya mwanadamu.
Wallahu aalam.

Ameyaandka
Khamis Alghammawi

Read 3945 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Add comment


FaLang translation system by Faboba