113: AFANYE NINI ILI AONDOKANE NA HASADI?

Written by

Assalaam aykum warahmatullah wabarakaatuh

kuna ndugu yetu ni mfanyabiashara ilikua biashara yake ikienda vizuri ila katika miaka mitatu iliopita amepata misukosuko ya kuchukuliwa pesa kwa njia za kimazingara (uchawi) na hadi sasa amekuwa na deni kubwa ambalo hawezi hata kulilipa anaomba asaidiwe atumie njia gani ili asalimike na hasadi, hiyo na aweze kurudisha biashara na pesa za watu?

Yaani nakusudia dua zipi anatakiwa afanyiwe ili kama kuna anaemchukulia hiyo pesa aache?

JAWABU:
Waalaykm salaam warahmatullah wabarakatuh.

1. Kithirisha Istighfaar sana na kuomba touba kwa Allah mtukufu isije kuwa ni adhabu kutoka kwa Allah mtukufu kutokana na baadhi ya makosa aliyonayo mja.

2. Jilazimishe kusoma Adhkaar za asubuhi na jioni. Kisha kumuomba Allah mtukufu baada yake akufungukie kheri za siku hiyo na akukinge na shari zake.

Alamnasharaha ×7
Qulhuwallahu ×7
Suuratulfalaq ×7
Suuratunnas ×7
Aayatulkursiyy ×7

Bila kusahau adhkaar za baada ya sala. Hasa Aayatulkursiyy, Qulhuwallah, Suratulfalaq na Suratunnas Mara moja moja ispokuwa Magharb na Alfajri inakuwa Mara tatu tatu, na Subhaanallah wabihamdihi ×100

Pia soma au weka recording ya Suratilbaqara daima katika sehem yako ya kuwekea pesa kwani Suratil baqara huwafukuza masheitani. Kama ilivyokuja katika hadithi.

Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis Alghammawi

Read 4043 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Add comment


FaLang translation system by Faboba