Ibadhi.com

110: NINA MATATIZO KATIKA MAISHA

You have a new Question by:

Ahil Haroon from

Tanzania

--------------------------------------

Swali:

1. Nampenda mwanamke lakini simpati na huwa tunagombana
2. Watu huwa wananichukia sana
3. Kitu chochote nikifanya huwa inaharibika
4. Nikipata pesa huwa hazikai mkononi ila zinapotea nakua sijui nimetumia wapi
5. Mimi ni mwanaume lakini na matatizo sehemu ya siri
6. Mimi huwa napata ndoto mbaya sana wakati nikilala mpaka natoka na manii
7. Mimi nina shida na maisha yangu badala ya kwenda mbele narudi nyuma.

JAWABU:
Waalaykm salaam warahmatullah wabarakatuh.

 Jumla ya nasaha zifuatazi zinaweza kukufaa.

1. Rekebisha mahusiano yako na mola wako, kwa kufanya touba ya kweli na kuacha kila maovu pia kusoma Quran na kujilazimisha na adhkaar za kila pahala kama kulala, kula, n.k. Pamoja na kujikurubisha kwake kwa Ibada hasa sala, Funga na kutoa Sadaka.

2. Fungua akaunti benki ya kiislam, na ukipata pesa kaziweke huko.

3. Weka mipango ya matumizi yako ya kila mwezi ili kuzuia kununua visivyokuwemo katika budget. Pamoja na kuandaa sehem nyingine ya kuandika kila matumizi.

4. Kama hujaoa basi fanya Istikhara umuombe Allah mtukufu akusahilishie ikiwa ni kheri kwako na akuepushie ikiwa ni shari kwako, kisha penda kilichopo kama ulichokipenda hakipo.

5. Jihadhari na waganga watakutapeli.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment