Ibadhi.com

109: ZAKA YA DENI

 

You have a new Question by:

Hafiid Muhammad from

Tanzania

--------------------------------------

Swal

 

Hafiid Muhammad from

Tanzania

--------------------------------------

Swali:

Assalamu alaykum


Ninauliza hivi "mali iliyokopeshwa kwa mtu ikiwa imefika nisaab na ikafika muda wa kutoa zaka je mkopeshaji anatakiwa kuitolea zaka hali ya kuwa hajarudishiwa mali yake hiyo?"

JAWABU:
Waalaykm salaam warahamtullah wabarakatuh.

Deni au mkopo ukitimiza mambo matatu basi itamuwajibikia Yule anayedai atolee yeye Zaka amma ikipungua moja kati ya hayo matatu au mawili au yote basi itamlazimikia anayedaiwa.

Mambo hayo:
1. Imefika muda wake wa kulipwa.
2. Aliyekopeshwa awe muaminifu mlipaji.
3. Aliyekopeshwa awe na Mali ya kulipia hilo deni.

Yakitimia hayo hata kama ile Mali hajapewa bado basi itamuwajibikia aiweke katika hesabu ya Zaka zake kwa mwaka ule.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment