Ibadhi.com

107:MTU MWENYE MATATIZO YA KUTOKWA NA UPEPO,JE ASOME QURAN?

Munira Miraji from

Tanzania

--------------------------------------

Swali:

Je inaruhusiwa kwa mtu aliye na matatzo ya kutokwa na upepo kusoma Quran baada ya swala ya faradhi au sumna?

JAWABU:
Waalykm salaam warahmatullah wabarakatuh.

Wanachuoni wametofautiana kuhusu mtu asiyekuwa na udhu (Uchafu mdogo)  kusoma Qur an tukufu.
Wapo walioruhusu moja kwa moja baada ya kuona kutothibiti au kutokuwepo kwa hoja katika dalili zitolewazo na wenye kukataza.

Wapo waliokataza moja kwa moja kwa dalili walizoziona zimethibiti katika sunnah na wengine wakatoa dalili katika Quran kwa aya :
(لَا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ)
'Hawaigusi Quran ispokuwa waliotakaswa"
[Surat Al-Waqi'ah 79]

Amma hadithi ni kwa aliyoyapokea Imam Rabii katika Musnad yake:
11) ... أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ قَالَ: قَالَ رَسُول اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْجُنُبِ وَالْحَائِضِ وَالذِينَ لَمْ يَكُونُوا عَلَى طَهَارَةٍ: «لاَ يَقْرَؤُونَ الْقُرْآنَ، وَلاَ يَطَؤُونَ مُصْحَفًا بِأَيْدِيهِمْ حَتَّى يَكُونُوا مُتَوَضِّئِينَ».
Abu Ubaidah kutoka Jabir bin Zaid Amesema: Amesema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- kuhusu wenye janaba na wenye hedhi na wasiokuwa na udhu : wasisome Quran,  sala wasiukamate kwa mikono yao mpaka wawe wana udhu- wamesafika-"

Na bila shaka dalili hii iliothibiti inaipa nguvu qauli ya waliokataza.

Na wapo waliopita njia ya kati kati wakaona kuwa katazo ni la hadathi kubwa (Janaba, Hedhi,  na Nifasi)  Amma kutokuwa na udhu kikawaida basi inapendelewa atie udhu kabla ya kusoma au kushika Qur-an.

Pamoja na khilafu lakini wanachuoni wanasema dharura na hali tofauti zina hukmu zake.
Wakatoa ruhusa kwa wanafunzi wadogo w a Qur an ambao wanapata tabu ya kutia udhu kila Mara, kupitia mlango :
(وَجَاهِدُوا فِي اللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ  مِلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِنْ قَبْلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ)
[...Allah mtukufu hajaweka juu yenu uzito katika dini...]
[Surat Al-Hajj 78]

Na aliposema katika aya ya udhu:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ مِنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُمْ مِنْ حَرَجٍ وَلَٰكِنْ يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ)
[…Allah mtukufu hataki kukuwekeeni uzito juu yenu lakini anataka kukutakaseni na akutimizieni neema yake juu yenu ili mshukuru"
[Surat Al-Ma'idah 6]

Na ni kupitia msingi huo wanachuoni wamemruhusu mwenye mkojo au damu au kutokwa na upepo kwa kuendelea kusali faridha, sunnah na kusoma Quran kwa udhu ule wa sala husika kwa vile ni jambo zito kwake kutia udhu kila akitokwa na chochote katika hayo niliyoyatanguliza.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment