Ibadhi.com

106:DUA YA KUKUBALIWA MAOMBI YAKO HARAKA KWA ALLAH MTUKUFU

Bizabishaka Aisha from

Burundi

--------------------------------------

Swali:

Duwa gani ao aya gani ndani ya qur'an Unaweza kuitumiya kutaka ALLAH akubali maombi yako haraka. Na unaweza ku swaum siku ngapi?

JAWABU:

Dua ndio msingi wa Ibada, Allah mtukufu ametutaka tuelekee kwake moja kwa moja tuombapo dua zetu.

Akasema :

((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ ))

?? Na amesema Mola wenu: Niombeni nitakujibuni??

Kisha akabainisha ya kuwa yeye yupo karibu nasi kuliko tinavyofikiri akasema :

(وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ)

??Na watakapokuuliza waja wangu kuhusu mimi: basi mimi nipo karibu, hujibu maombi ya muombaji aniombapo, basi waniitikie mimi na waniamini ili wapate kuongoka??

[Surat Al-Baqarah 186]

Pamoja na hayo, Allah mtukufu hajaweka baina yake sababu wala nasabu yenye ukaribu kama uchamungu, Wachamungu wakitakacho hupewa, waliombalo hujibiwa, walisemalo husikilizwa, basi Njia bora ya kukubaliwa maombi yetu ni kuwa wachamungu, Amesema Allah mtukufu:

(وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ)

??wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa haki, pale walipotoa vikurubisho basi kikakubaliwa -kikurubisho- cha mmoja na kingine hakikukubaliwa, akasema-yule ambaye hakukubaliwa- nitakuua, Akasema yule -aliyekubaliwa- : Hakika Allah mtukufu huwakubalia wachamungu tu.??

[Surat Al-Ma'idah 27]

Maneno haya yametiliwa mkazo na Bwana Mtume Muhammad -Sallallahu alayhi wasallam- aliposema:

اللهَ قال ، ...وما تقرَّب إليَّ عبدي بشيءٍ أحبَّ إليَّ ممَّا افترضتُ عليه ، وما يزالُ عبدي يتقرَّبُ إليَّ بالنَّوافلِ حتَّى أُحبَّه ، فإذا أحببتُه : كنتُ سمعَه الَّذي يسمَعُ به ، وبصرَه الَّذي يُبصِرُ به ، ويدَه الَّتي يبطِشُ بها ، ورِجلَه الَّتي يمشي بها ، وإن سألني لأُعطينَّه ، ولئن استعاذني لأُعيذنَّه >>

Allah mtukufu amesema: Hakuna jambo ninalolipenda zaidi kwa mja wangu kujileta karibu yangu kuliko yale niliyomfardhishia, na ataendelea kusogea karibu yangu kwa ibada za ziada (Sunnah) mpaka nitampenda, Nikishampenda nimuwafiqisha katika maskio yake anayosikizia, macho yake anayo onea, mikono yake anayoshikia, na miguu yake anayotembelea, -katika utiifu-, Ikiwa ataniomba nitampa, na akijikinga kwangu nitamkinga" Bukhari 6502

Pia Allah mtukufu ametutaka tumuombe kwa majina yake na sifa zake tukufu aliposema :

(قُلِ ادْعُوا اللَّهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَٰنَ ۖ أَيًّا مَا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا)

??Sema: Muiteni Allah mtukufu au muiteni Alrahmaan, lolote mtakalotumia kati ya hayo yeye anayo majina mazuri matukufu,...??

[Surat Al-Isra' 110]

Pia amesema :

(وَلِلَّهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ)

??Allah mtukufu anayo majina mazuri basi muiteni/muombeni kwa majina hayo...??

[Surat Al-A'raf 180]

Katika hadithi amesema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-

"إنَّ للهِ تسعةً وتسعين اسمًا ، مائةً إلا واحدًا ، من أحصاها دخل الجنةَ ."

??Hakika Allah mtukufu ana majina tisini na tisa, Mia moja kasoro moja, atakaeyahifadhi ataingia peponi??Bukhari 7392.

Pia Allah mtukufu ametujulisha katika njia za kuomba dua ni baada ya kumaliza kufanya amali yoyote ya kheri, Kama sala, kusoma quran, kutoa sadaka n.k. kwa qauli yake:

(فَإِذَا فَرَغْتَ فَانْصَبْ)

??Utakapomaliza -ibada- basi jichokeshe -katika kuomba dua-??

[Surat Al-Sharh 7]

Wamesema baadhi ya wanachuoni : "Anayemaliza sala kisha asiombe dua ni kama mtu aliyetikisa mti wa matunda yalipodondoka akaondoka bila kuyachukua"

Pia wakati wa kuteremka mvua, wakati wa kabla ya alfajiri, wakati wa baina ya adhana na Iqama, Lailatul qadri n.k.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:

Khamis bin Yahya Alghammawi

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment