Ibadhi.com

105: TALASIMU

 

issa haruna from

Tanzania

--------------------------------------

Swali:

je talasimu ni halali katika dini maana kuna talasimu kama za mvuto wa biashara je zinafaa kutumia ?

JAWABU:
Allah mtukufu ametuamrisha tumuombe yeye katika kila tukitakacho katika maisha ya dunia.
Amesema :
(وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ)
Na Amesema mola wenu: Niombeni nitakujibuni, hakika wale ambao wanafanya kibri kunako ibada yangu wataingia motoni kwa udhalili.
[Surat Ghafir 60]

Na riwaya zimekuja nyingi zenye kuonyesha kuwa bora ya Ibada ni mtu kujiombea mwenyewe, na mwenye kushindwa kuliko wote ni aliyeshindwa kujiombea dua mwenyewe.

Hivyo inapendelewa kwa muislam kuishika nguzo hii muhimu, pamoja na kutazama kwake nyakati ambazo kisheria zimependelewa katika kuomba dua iliyo muhimu katika zote ni kila baada ya wema, mfano: kila baada ya sala, kila baada ya kutoa sadaka, kila baada ya kusoma Qur an n.k.

Kwa Msingi huu Talasimu kama yenyewe haina uwezo wa kuleta manufaa wala kuondodha madhara, haiponyi wala haikingi, Mwenye kuitakidi tofauti na haya anaweza kuingia katika shirki, Allah mtukufu atukinge nayo.

Amma ikiwa talasimu hiyo imendikwa Quran au dua ya kawaida yenye kujulikanwa maana yake, Pamoja na usalama wa itikadi ya kuwa mwenye kunufaisha na kudhuru ni Allah mtukufu haikatazwi talasimu ya aina hiyo.

Amma ikiwa hiyo talasimu ni michoro isiyofahamika au maneno yasiyosomeka wala kujulikanwa au yenye kujulikanwa maana yaka lkn ikawa kuna kumuomba asiyekuwa Allah mtukufu kama majini au malaika basi itakuwa haifai.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawy
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment