Ibadhi.com

104: DUA YA KUMRUDISHA MTU ALIYEPOTEA.

issa haruna from 

Tanzania

--------------------------------------

Swali: 

Dua gani isomwe kumrudisha mtu aliyepotea ? 

JAWABU:

Waalkm salaam warahmatullah wabarakatuh.

 

Qur an yote ni ponyo na Rehma kama alivyoeleza Allah mtukufu :

(وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِلْمُؤْمِنِينَ ۙ )

《Na tunateremsha Quran ambayo ni ponyo na Rehma kwa waumini》

[Surat Al-Isra' 82]

 

Na imepokewa kuwa Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- amesema

"اقرؤوا القرآنَ ، و سلوا اللهَ به"

《Someni Quran, na muombeni Allah mtukufu kwa Quran hiyo》

 

Na katika baadhi ya athari zilizopita wamesema :

 "خذوا من القرآنِ ما شئتم لما شئتم"

《Chukueni katika Qur an mkitakacho kwa muyatakayo》

 

Kwa Misingi hiyo Sura yoyote katika Quran ukaichukua na kuisoma kwa Ikhlas na yaqini kisha ukqmuomba Allah mtukufu basi Allah mtukufu atakupa ukitakacho.

 

Na katika Sura ambazo tumeskia wengi wakizisoma Suurat Yasin, pia wakirudia rudia vaya zifuatazo:

حسبنا الله ونعم الوكيل

"Hasbunallahu waniimal wakiil"

au

"فسيكفيكهم الله وهو السميع العليم"

"Fasayakfiikahumullah wahuwa samiul aliim"

Bila kusahau kuamka usiku na kusali rakaa za kumumomba Allah mtukufu kwani nyakati hizo dua hujibiwa.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:

Khamis bin Yahya Alghammawi

? Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment