Ibadhi.com

103: NAMNA YA KUSALI SALA YA DHUHA ?

Mohammed Al - Hashmy from 

Tanzania

--------------------------------------

Swali:

As salaam alaykum warahmatullah wabarakatuh. 

Mimi naomba mtufunze jinsi ya kuishwali hii swala ya Dhuhaa. 

Ahsante shukran.

 

JAWABU:

Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

 

Sala ya dhuha ni sala ya Sunna inayosaliwa katika muda wa baada ya kuchomoza jua lote mpaka kabla ya kufikia jua kati kati ya anga.

 

Ikisaliwa mapema huitwa Ishraaqi kwa jina lingine, Ikisaliwa taqriban saa nne kiswahili (Saa kumi oman) inakuwa bora na ikicheleweshwa pia inajuzu.

Bora ya rakaa zake ni nane

 197) ... أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ قَالَ: بَلَغَنِي عَنْ أُمِّ هَانِئٍ بِنْتِ طَالِبٍ قَالَتْ: صَلَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بَيْتِي صَلاَةَ الضُّحَى ثَمَانِيَ رَكَعَاتٍ>>

Amesema Ummu haani bint Taalib :

《Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- alisali nyumbani kwangu sala ya dhuha rakaa nane》

Lakini inajuzu kusali rakaa mbili, au nne au sita n.k.

Nayo husaliwa rakaa mbili mbili kwa kutoa salam baina yake.

Nayo ndiyo huitwa sala ya waliotangulia au waliorejea kwa Allah mtukufu.

Baadhi ya riwaya zajulisha kuwa wenye kuisali watakuwa na malipo yao maalumu siku ya Qiyama.

Wallahu aalam.

 

Ameyaandika:

Khamis Alghammawi

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment