Ibadhi.com

102: MUME HAMSHUGHULIKII MKEWE KWA MIEZI SITA SASA HIVI ?

SHAFI SHAFI from 

Kenya

--------------------------------------

Swali:

mume ameteta na mkewe hapiti wala hamshuhulikii miezi sita sasa je ndoa iko ?

JAWABU:

Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

 

NDOA IPO.

 

Lakini mke ana haki ya kuomba kuachwa, kwa vile hatimiziwi haki zake, na kama mume atakataa basi alipeleke jambo la kwa Kadhi ambaye Sheria imempa uwezo wa kumuandikia talaka hata kama mume atagoma.

 

Na wote wawili wamuogope Allah mtukufu, wasikiache kibri kikaharibu ndoa yao, waombane msamaha, warudi kama zamani. Allah mtukufu anasema kuwaambia wanamme :

 (...وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَنْ يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِنْ كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا)

Wala msiwadhiki wanawake ili mpate kuchukua vile mlivowapa, Ispokuwa kama wataleta uovu uliowekwa wazi, na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mtawachukia basi huenda mkachukia jambo na Allah mtukufu akajaalia ndani yake kheri nyingi"

[Surat An-Nisa' 19]

 

Na Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- amewausia wanawake wasiwe wenye kuzikana neema za waume zao, aliposema :

>

《 Nimeona Wengi katika watu wa motoni ni wanawake. wakasema : kitu gani kinachosababisha ewe Mjumbe wa Allah ? Akasema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-: Kwa kukufuru kwao, wakasema: Je wanamkufuru Allah mtukufu ? Akasema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-: Wanakufuru mahusiano mazuri, law kama utamfanyia wema mmoja wao zama zote kisha akaona kwako jambo moja - hakulipenda- atasema: Sijaona kheri yoyote kwako"

 

Na Allah mtukufu amewanasihi wote kwa kusema :

( ۚ وَلَا تَنْسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)

Wala msisahau fadhila zilokuwa baina yenu, Hakika Allah mtukufu ni muoni kwa myafanyayo.

[Surat Al-Baqarah 237]

 

Na mengi ya matatizo ya ndoa yanaanzia katika kuchagua basi tunawaomba wazingatie wanamme na wanawake haya mambo ya ndoa katika dini.

Wallahu aalam.

 

Ameyaandika:

Khamis Yahya Alghammawi

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment