Ibadhi.com

101. KUBAKIA NA MURTADI KATIKA NDOA

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

SUALI:

Mume wangu ameritadi na kuacha Uislamu ni ipi hukumu ya doa yetu?

Tunaomba jawabu kwa dalili.

JAWABU:

Allah mtukufu ameharamisha doa baina ya Muislamu na Mshirikina kama alivotueleza katika Kitabu chake:

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

Na musioe wanawake washirikina mpaka waamini, na mjakazi muumini ni bora kuliko mwanamke mshirikina hata akikupendezeni, na musiwaozeshe wanaume washirikina mpaka waamini, na mtumwa muumini ni bora kuliko mwanamme mshirkina hata akikupendezeni. Hao wanaita katika Moto, na Allah anaita katkika Pepo na usamehevu kwa idhini yake, na anabinisha aya zake kwa watu ili wakumbuke. (Al-Baqarah 221)

Vile vile Allah mtukufu anatuambia:

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

Hao (wanawake waumini) si halali kwao hao (wanaume washirikina), na hao (wanaume washirikina hawawi halali kwao hao (wanawake waumini). [Mumtahina 10].

Na kwa maana hiyo muislamu hawezi kubakia na mshirkina katika doa kamwe.

Likibainika hili itakulazimu uachane nae huyo Murtadi aliyeacha Uislamu na kuingia katika mila nyengine ya Kishirkina au ya Kupingamungu, kisha utakaa eda, na baada yake akitokezea mume muislamu mposaji unaweza kuolewa nae.

Wallahu aalamu.

 

 

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment