Ibadhi.com

94:JE KUPIGA PUNYETO NI SAWA NA KUZINI NA MAMA MZAZI ?

JE KUPIGA PUNYETO NI SAWA NA KUZINI NA MAMA MZAZI ?

You have a new Question by:

khalfan khu from

Oman

--------------------------------------

Swali:

Asalam alaikum warahmatullahi wabarakatuhu
suali langu ivi nikweli watu wanao jichuwa yani kupiga punyeto nikama wamezini na mama zao wazazi ?

JAWABU:

Waalykm salaam warahmatullah wabarakatuh.

Bila shaka kupiga punyeto ni katika madhambi makubwa yanayowatesa vijana wengi ambao hawajaoa.

Na hapana Shaka kuwa madhara yake kiafya yapo wazi kama ;

1. Kupoteza hamu ya kufanya tendo hilo kawaida.

2. Kulegeza misuli ya sehem za siri na kupelekea kukosa uwezo wa kumuingilia mwanamke.

3. Inapunguza uwezo wa kufaham kwa sababu upandishaji wa hisia unaendana na sana na mishipa ya faham na hivyo kupoteza nguvu nyingi katika lisilo na tija na lisilo na uhalisia.

4. Kupoteza kujiamini na kujihisi unyonge wa daima na upweke, hili hupelekea msongeko wa mawazo hali ambazo hupelekea mtu hata kujinyonga wakati mwingine.

5. Hupatwa na tatizo la kutokwa na Manii au Madhii bila taarifa, kutokana na ulegevu wa misuli yake.

6. Wanakuwa katika hatari ya kuingia katika Ushoga (Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile kwa wanaume), kwa kuathirika akili yake na njia ziziso salama za kumfikisha katika starehe na hasa baada ya kupoteza uwezo wa kuingilia kikawaida.

Amma kisheria; Bila shaka Punyeto ni haram kwanza kwa madhara tuliyoyataja hapo juu lakini pia kwa sababu si njia ya kisheria ya kumaliza matamanio, Amesema Allah mtukufu:

(وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ * إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ * فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ)
"Na waumini ni wale ambao ni wenye kuzihifadhi tupu zao, Iapokuwa kwa wake zao au wajakazi wao hapo si wenye kulaumiwa. Basi atakayetaka tofauti na hayo ndio maadui"
[Surat Al-Mu'minun 5 - 7]

Na Mtume -sallallahu alayhu wasallam- Amewaelekeza vijana njia mbili, Imma kuoa au kufunga ili kuvunja matamanio.

Na Maulamaa huita punyeto ni kuua viumbe hai kulikojificha.


Kwa hivyo Muislam ajiweke mbali na vitendo hivi viovu, amuogope Allah mtukufi na ajue kuwa ataulizwa kuhusu neema anayoipoteza kwa mkono wake.

Amma kuhusu kulingana kwake na kumuingilia mama mzazi, Sijaona pahala palipoandikwa hayo..

Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis bin Yahya Alghammawi

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment