Ibadhi.com

85. AFANYE NINI ASIYEWEZA KUCHUNGA UDHU ?

Swali:

Assalam Alaykum. Afanye nn asieweza kuchunga udhu, mda mwengine unatenguka Kati Kati ya swali msaada wenu tafadhali.

JAWABU:
Waalaykum salaam.

Asiyeweza kuchunga udhu kwa kutoweza kujizuia kutokana na maradhi aliyonayo kama kutokwa na haja ndogo mfululizo, Au upepo kiasi hawezi kujizuia kwa kulegea misuli inayozuia hilo kwanza aende hospitali ili apate tiba ya maradhi yake hayo.

Amma yanayohusiana na Sala yake:

- Ikiwa anapata fursa ya wakati ambao udhu wake hautenguki kiasi cha yeye kuweza kusali na kumaliza basi atasubiri wakati huo, Ili asali muhimu muda wa sala usipite wote naye hajasali.

- Ikiwa hapati muda huo - yaani wakati wote yeye anakuwa katika najasa - basi hapo maulamaa wanasema atajisafisha ikikaribia karibu na sala kisha ataweka chenye kuzuia ile najisi kufika katika nguo zake za nje, kisha atatia udhu na atasali mpaka amalize.

- Udhu wake atautia kwa niya ya kuhalilikiwa kusali kama walivyosema kundi kubwa la wanachuoni.

- Amepewa ruhusa ya kukusanya sala mbili kwa pamoja ((Adhuhri na Asri)) au ((Maghribi na Isha)) katika wakati wa moja ya sala mbili hizo bila kurudia udhu wake.

- Akisali kila sala peke yake basi itanlazimikia kutia udhu kwa kila sala.

Na Asili ya hukmu katika mlango huu ni yaliyopokelewa na Bukhari 228, Muslim na wengineo kuwa Mtume sallallahu alayhi wasallam alisema Kuhusu mwanamke (Fatma bint Hubaishi) ambaye damu yake inaendelea kutoka bila kukatika "Hiyo ni damu ya mshipa, zikianza siku za hedhi yako acha kusali zikimalizika sali" Amesema Ur'wa "Kisha atakuwa anatia udhu kwa kila sala"

Amesema Bii Aisha Mama wa waumini - Allah mtukufu amridhie - "Mmoja wa wake wa Mtume -sallallahu alayhi wasallam- Alikaa naye Itikafu, Ikawa anapata damu na umanjano, ikawa ana sali" Bukhari

Na amepokea Bii Aisha pia kiwa Ummu Habiiba alipata damu ya Ugonjwa miaka saba, Akamuuliza Mtume - sallallahu alayhi wasallam- Mtume akasema " Hiyo ni damu ya mshipa" na alikuwa Ummu Habiba anatia udhu kwa kila sala" Bukhari 327.

Wallahu aalam.
Khamis Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment