Ibadhi.com

68.HUKMU ZA FUNGA NA MAANA YA IFRAAD

Assalam alykum 

SWALI: 

Ni zipi hukmu za fungal ? 2) ifraad ni aina gani ya hija na inahusika na matend gani ?

JAWABU:


W/salaam.

Funga inaweza kuwa na hukmu tofauti kutokana na aina yake:

1. Waajib ((Lazima)) nayo ni Funga ya Ramadhani, Funga ya Kafara, na Funga ya Nadhiri.

2. Manduub ((Sunnah)) nazo ni nyingi mfano Shaaban, Jumatatu na Alkhamis, siki nyeupe ((13,14,15)) za kila mwezi wa kiislamu n.k.

4. Karaha mfano kufunga mwezi 11, 12, na 13 ya mwezi dhulhijjah.

5. Haram kam kufunga siku za Eid, au kwa mwenye Janaba na Hedhi n.k.

Amma Ifraad ni hali ya mtu kwenda Kuhiji tu pasina kufanya na Umra katika safari yake hiyo.
Na vitendo vyake ni vitendo vyote wanavyofanya Mahujjaaj. Unaweza kurejea sehem ya Fiqh katika Website yetu ibadhi.com utaona vitendo vya Mahujjaj.
Aina nyingine za Hijaa ni Qiraan na Tamattui.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu


Khamis bin Yahya Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
12 Dhulhajj 1438h
3 September 2017m

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment