Ibadhi.com

60:ANA MARADHI YA ANEMIA

ANA MARADHI YA ANEMIA

You have a new Question by:

Mishi Athman from

Kenya

--------------------------------------

Swali:

Assalam Alaykum, Mwenye ugonjwa wa upungufu wa damu (anaemia) ashindwa kufunga katika mwezi wa Ramadhan. Je siku atakazokosa kufunga itamlazimu kulipa? na kama bado hali ya afya haimuwezeshi kufunga ipo njia nyengine ya kulipa swaum kando na kufunga?

Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Allah mtukufu awape sihha na afya njema wagonjwa wetu, hakika yeye ni muweza wa hayo.

Allah mtukufu amewapa wagonjwa na wasafiri katika mwezi wa Ramadhani ruhusa ya kula mchana wa Ramadhani kwa kulazimika kulipa pale watakapopowa. Akasema Subhaana.

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Allah mtukufu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Allah mtukufu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.

((Sura Al-Baqarah, Ayah 185))

Lakini katika dhahiri ya maradhi yapo maradhi mepesi ambayo mtu anaweza kufunga wala hakuna hatari yoyote itakayompata kwa kufunga... Basi huyo bado hajapewa ruhusa ya kula kwa Qauli ya Allah mtukufu :
فَاتَّقُوا اللَّهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنْفِقُوا خَيْرًا لِأَنْفُسِكُمْ ۗ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

Basi mcheni Allah mtukufu kama mwezavyo, na sikieni, na t'iini, na toeni, itakuwa kheri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio walio fanikiwa.
((Sura At-Taghabun, Ayah 16))
Na bila shaka swaumu bado imo ndani ya uwezo wao.
Pia yapo maradhi ambayo hayapou kabisa kwa mujibu wa taqrir za Matabibu makhsusi wa maradhi hayo, na hayamuondoki mwanadamu mpaka mwisho wa uhai wake, na ikawa ni mazito hawezi mgonjwa kufunga ispokuwa hatari ya kuzidi maradhi hayo na Kifo, vitakuwa vimemfikia, basi Uislam umeweka njia ya kulisha chakula kwa kila siku ya Ramadhani, Amesema Allah mtukufu:

أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ ۚ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَنْ تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ ۚ وَأَنْ تَصُومُوا خَيْرٌ لَكُمْ ۖ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ

(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.

((Sura Al-Baqarah, Ayah 184))

Kwa hivyo ayapime maradhi hayo ya Anemia katika vigawanyo hivyo tulivyovitaja. Na pale yatakapokaa ndio itakuwa hukmu yake.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis Bin Yahya Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
17 Shawwal 1438h
12 July 2017m
Zanzibar - Tanzania.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment