Ibadhi.com

57:MASTERBATION INAFUNGUZA

MASTERBATION INAFUNGUZA


You have a new Question by:


athumani mohamedi from

Uganda
--------------------------------------


Swali:
marstabetion ina mfunguza saumu.

JAWABU:
MASTER BATION ni katika madhambi makubwa yaa uuaji wa kiuficho.

Pia ni kupoteza neema ya mbegu za uhai, alizotupa Allah mtukufu.

Nimesema katika moja ya majibu :

"Allah mtukufu atukinge na shari hii yenye kuangamiza duniani kwa :

1 - kupoteza nguvu za kiume
2 - kupoteza nguvu za macho
3 - inaleta msongo wa mawazo
4 - Kuleta matatizo ya kufahamu
5 - inayoua kizazi, na kusababisha mtu kukosa uzazi kabisa au kupata kwa tabu kubwa.
6 - mupoteza wakati ambao law ungetumiwa vizuri ungekiwa na tija njema.
7 - kupoteza nguvu ya kifikra na kiuchumi
8 - kiwa na hasira za haraka.

Na maafa mengine mengi.

Pia yaleta machukizo ya Allah mtukufu, kwa vile tendo hilo halina tofauti na wale walokuwa wakiwaua watito wao wa kike kwa kuhofia ada na desturi za jamii zao, hivyo kila tone moja la manii linalopotezwa kwa njia hiyo binadam ataulizwa kuhusu hilo, na wapi atapata jawabu ya maswali hayo ❓

وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ
بِأَيِّ ذَنْبٍ قُتِلَتْ

Na aliye zikwa hai atapo ulizwa,Kwa kosa gani aliuliwa?

Pia ataulizwa vipi aliipoteza neema hiyo inayotakiwa iwe kwa wanawake mpaka wanne alowekewa kisheria,

فَانْكِحُوا مَا طَابَ لَكُمْ مِنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا

Basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana. 04:03

Na bila shaka kupiga punyeto ni uadui wa wazi kwa ubinadamu, na tabia ya kisheitan, na ni mwisho wa dhulma ya kijamii. Amesema Allah mtukufu:

(وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ * إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ * فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ)
Na ambao wanahifadhi tupu zao. Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka.
[Surat Al-Ma'arij 29 - 31]"
Mwisho wa kunukuu.

Na katika jawabu yangu nyingine, ilikuwa :

Swali:
Salam alykum
Naomba kuuliza mtu ambae anae jitoa shahawa au anae fanya masterbution na akaoga janaba anaruhusiwa kufunga

JAWABU:

Subhaanallah... Allah mtukufu aturuzuku touba ya kweli. Hivi atamueleza nini mola wake mtu huyu ? Au anajiona mjanja kwa kubaki hai mpaka sasa ? Haoni ni fadhila kubwa kapewa kuudiriki mwezi huu wa Ramadhan ?

Subhanallah...!!!

Amma kuruhusiwa, naam anaruhusiwa bali ni wajibu kwake kama ilivyo kwa wengine, na kama atafanya huo uchafu wake wakati wa mchana atalazimika kuilipa hiyo siku na kufunga miezi miwili mfululizo baada yake.

Na ajue pamoja na kulazimika huko, malipo ya funga yatamfaa ikiwa tu atatubia na kuacha dhambi zake na kurudi kwa mola wake, kama hakutubia na akakutwa na mauti atakuwa hana malipo ispokuwa moto wa Jahannam wa milele bila kutoka wala kupunguziwa.

Allah atukinge na khidhlan, aturuzuku Toubah kabla ya mauti na atukubalie touba hiyo.
Wallahu aalam.
Mwisho wa kunukuu.

Na hukmu yake katika swaumu ni sawa sawa na hukmu ya mzinifu au mwenye kumuingilia mkewe mchana wa Ramadhani.

Inafunguza swaumu, na inawajibisha kafara ya kufunga miezi miwili mfululizo akiyafanya hayo mchana pamoja na toba, Na ikiwa ni usiku basi inazuiwa kukubaliwa kwa amali yake hiyo mpaka atubie kwa Allah mtukufu.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis Bin Yahya Alghammawi
10 July 2017.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment