Ibadhi.com

51: KUVAA JAMBIA KABLA YA KUGAWIWA URITHI

Rashid Mahrooqi from

Oman
--------------------------------------
Swali:

Nini hukumu ya kuvaa jambia bila kuuliza wanao husika katika urithi wa ile mali ?

JAWABU:
Uislam umeweka utaratibu wa namna ya kutumia mali ya mwengine lazima iwe kwa ridhaa ya mwenye mali.

Na binadam muislam anapofariki mali inakuwa ni ya warithi wake, kila mmoja analo fungu lake kapewa na mola wake kama ulivokuja utaratibu katika Suurat Nisaa aya 11 na 12 na aya ya mwisho.

Na inakatazwa kuchukua mali ya wengi kabla ya ugawaji ikiwa yeye yumo katika warithi au wenye kustahiki, na inahesabiwa kuwa hiyo ni ghuluul (( khiyana)) ambayo imekatazwa katika Qur an aliposema Allah mtukufu:

وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَنْ يَغُلَّ ۚ وَمَنْ يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana. Na atakaye fanya khiyana, atayaleta Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila mtu atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa.

-Sura Aal-E-Imran, Ayah 161.

Pia katika hadithi Mfanyakazi wa Mtume sallallahu alayhi wasallam ulipomjia mshale na kumuua, Masahaba wakamfurahikia kuwa ameipata pepo kwa kuwa kwake katika Jihaad.
Mtume akasema : " Hakika shuka aloichukua kabla ya kugawa mali tulizopata vitani inamuwakia moto"

Basi hiyo ndiyo hali shuka basi vipi itakuwa Jambia ?

Na hiyo ndiyo hali ilompata swahaba aliyefia vitani basi vipi sisi?

Amepokea Imam Rabii katika Musnad yake hadithi no 660 kuwa Mtume - Sallallaahu alayhi wasallam-
"Atakayejichukulia haki ya Muislam kwa kiapo cha Uongo, Allah mtukufu amemuharamishia pepo na amemuwajibishia moto" akasema mtu mmoja "hata kitu kidogo ewe Mjumbe wa Allah ?" Akasema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-: "hata ikiwa ni mswaki wa mti"

Amma ikiwa watamridhia warithi wote hakuna katazo kwa sababu ni mali yao, na bora mirathi igawiwe ili kila mmoja abakie na mali yake akiwa na milki kamilifu ya matumizi.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu:
Khamis bin Yahya Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
12 Ramadhan 1438h
8 June 2017m

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment