Ibadhi.com

49:KUMKUMBATIA MKEWE WAKATI WA MCHANA WA RAMADHANI.

 

Ally Akizimana from

28. KUMKUMBATIA MKEWE WAKATI WA MCHANA WA RAMADHANI.

Sweden

--------------------------------------
Swali:

Aslam aleykum
Swali langu nilikua nataka kujua inaruhusiwa kumshika,kumkumbatia mke wako katika mchana wa mwenzi wa Ramadhani?
Mvh Ally
JAWABU:
Waaleykum salaam warahmatullah wabaarakatuh.

Muislam ajiepushe na kila ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa swaumu yake.
Ajue hii ni fursa adhimu ambayo kupoteza siku moja ni msiba usioweza kupozwa na maombolezo ya zama zote.

Usiku upo na Allah mtukufu ameruhusu mke na mme kufanya yote wayatakayo katika waliohalalishiwa, Amesema Allah mtukufu:
أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَكُمْ وَأَنْتُمْ لِبَاسٌ لَهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَخْتَانُونَ أَنْفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنْكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنْتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Allah mtukufu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Allah mtukufu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Allah mtukufu, basi msiikaribie. Namna hivi Allah mtukufu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate kumcha.

{Sura Al-Baqarah, Ayah 187 }

Tazama aya hiyo ndugu yangu, yasema ni mipaka ya Allah mtukufu msiikurubie, basi vipi anajiaminisha na anakwenda kuchezea pesa karibia na lindi?

Swaumu ni kujizuia na matamanio.

Allah mtukufu atuwezeshe kufikia malengo ya swaumu, atukubalie, na atuweke katika watakaosamehewa na kustahiki pepo ya juu ya Firdaws.

Wallahu aalam.

Ameyaandika
Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
4 Ramadhan 1438h
30 May 2017m

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment