Ibadhi.com

48:KULA NYAMA YA SUNGURA

 

ALI SALEH from

Tanzania

--------------------------------------

Swali:

s'alaikum,
mm naoba kuuliza kuhu uhalali wa kula nyama ya sungura
Naomba ufafanuzi na kama ikiwezekana kuwe na ushahidi wa aya au hadithi .

Wabillahi taufiq

JAWABU:
Sungura ni mnyama kama wengine ambaye hakuna dalili ya kukataza kula nyama yake.

Na Allah mtukufu na Mtume wake -Sallallahu alayh wasallam- wametaja wanyama waloharimishwa na kuruhusu kila wasiokuwa haram.
Amesema :

(قُلْ لَا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَنْ يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنْزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَحِيمٌ)

Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Allah mtukufu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
[Surat Al-An'am 145]

Na kikawekwa kipimo cha ujumla cha vyakula vyenye kuliwa na vinywaji vya kunywewa kuwa vizuri visiwe vichafu.

يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُمْ مِنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ

Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyo kufunzeni Allah mtukufu. Basi kuleni walicho kukamatieni, na mkisomee jina la Allah mtukufu. Na mcheni Allah mtukufu; hakika Allah mtukufu ni Mwepesi wa kuhisabu.

{Sura Al-Ma'idah, Ayah 4}

Na Allah mtukufu amekataza kuharamisha hovyo, vile vizuri alivohalalisha

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ)
Enyi mlio amini! Msiharimishe vizuri alivyo kuhalalishieni Allah mtukufu, wala msikiuke mipaka. Hakika Allah mtukufu hawapendi wakiukao mipaka.
[Surat Al-Ma'idah 87]

Na Mtume Sallallahu alayh wasallam akatubainishia aina ya wanyama wasiofaa kuliwa akasema:
387) ... أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيءِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «أَكْلُ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنَ السِّبَاعِ وَذِي مَخَالِبَ مِنَ الطَّيْرِ حَرَامٌ».
Abuu Ubaida kutoka kwa Jabir bin Zaid kutoka kwa Abi Huraira kutoka kwa Mtume Sallallahu alayh wasaalam, amesema:
"Kula kila mnyama mwenye chonge au ndege mwenye kuwinda kwa kucha ni haram"

Na katika athari za wanachuoni wetu amesema sheikh Muhammad Alkindi - Allah mtukufu amrehemu- katika kitabu chake Bayaanu shar'i jz 7 uk 87 " Hapana ubaya kula nyama ya sungura"
Pia ametaja hivyo hivyo Sheikh Athumeini katika Taajul mandhuum.

Na wapo waliosema ni Makruhu kwa sababu inasemwa kuwa anapata hedhi.
Ametaja hayo Sheikh Shammakhi - Allah amrehem - katika kitabu al iidhaah jz 1 uk 330. Pia Sheikh Athumeini katika Taaj na Sharh nniil jz 1 uk 399

Na zimekuja baadhi ya riwaya kuwa Mtume aliletewa nyama ya Sungura, hakuila wala hakukataza kapokea Baihaqi na Abu Daawud.

Na zipo riwaya zingine zisemazo kuwa Abu Talha aliwinda Sungura, akamchinja akampelekea sehem ya nyama Mtume -Sallallahu alayh wasallam- akaikubali.
Bukhari 2572, Muslim 1953.

Amesema Imaam Qutbul aimmah - Allah mtukufu amridhie - katika Sharh nniil jz 2 uk 203 kuwa hiyo Qauli ya kuhalalisha ndiyo Qauli ya Imam Shaafi.

Dalili ni hizo, Wallahu aalam.

Amezikusanya
Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
4 Ramadhan 1438h
30 May 2016m

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment