Ibadhi.com

44. SUNNA YA KABLA YA MAGHARIBI.

Salim Bafagih from

Germany

--------------------------------------

Swali:

Assalam Aleykum
Huku ulaya kuzama kwa jua ni muda mrefu kuliko afrika na arabuni je inafaa kuswali sunna ya kablia baada ya adhana ya magharibi?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Kilichothibiti kwetu sisi ni kuwa Hakuna Qabliya kabla ya Magharibi.

Ispokuwa inajuzu kusali Nafla, kwani imetolewa ruhusa hiyo na Mtume s.a.w.
Kwani yeye alisema :
Salini kabla ya Magharibi, salini kabla ya magharibi, salini kabla ya Magjaribi Mkitaka.

Kwa hivyo inaruhusika kusali kabla ya Magharibj kwa nia ya nafla sio kwa nia ya Qabliya.

Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

09 April 2017m  

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment