Ibadhi.com

43: ZAKA YA ASIYESALI

Salim Bafagih from 

Germany

--------------------------------------

Swali:

Assalam Aleykum
1)Je Mtu asieswali zaka yake inakubaliwa ?

JAWABU:
Hakika Allah mtukufu ameweka sharti kuu za kukubali mema ya waja, sharti hiyo ni uchamumgu, amesema Allah mtukufu:

Akasema: Hakika Allah mtukufu huwapokelea wachamungu. Maida : 27

Kama ambavyo Allah mtukufu ameikutanisha Zaka na Sala sehemu moja, katika aya zote taqriban, hivyo kuviachanisha alivyovikusanya Allah mtukufu ni kuifanyia uadui zaka na sala kwa pamoja bali ni kumfanyia uadui Allah mtukufu na Mtume wake.
Amesema Allah mtukufu:

(وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ)
"Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mtume, ili mpate kurehemewa."
[Surat An-Nur 56]

Kama ambavyo Zaka inampa utakaso na usafi wa kumfanya ajue ukubwa na cheo cha sala na ibada zingine, Amesema Allah mtukufu:
(خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِمْ بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَهُمْ ۗ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ)

Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Allah mtukufu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua
[Surat At-Tawbah 103]

Kwa hivyo Zaka yake itakuwa ni imesimamishwa kukubaliwa kwake, akitubia madhambi yake mengine itakubaliwa na atapewa thamani ya malipo yake kamili bila kupunjwa, kama hakutubia yataporomoka yote aloyatenda katika wema. Anasema Allah mtukufu:
(أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ)
Je! Hawajui ya kwamba Allah mtukufu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaka, na kwamba Allah mtukufu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?
[Surat At-Tawbah 104]

TANBIIHI:
Haimaanishi maana hiyo kuwa awache kutoa yaliyomuwajibikia mpaka atakapoanza kusali, haasha wakallaa,...
Kwani atakapoacha atakuwa na deni, atakapotubia itambidi alipe na deni hilo la zaka kwa miaka yote itakayompita. Hivyo aendelee kutoa zaka, na amuombe Allah mtukufu tawfiiq ya kuweza kutekeleza ibada zote.

Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
09 April 2017m

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment