Ibadhi.com

35:Je ipo hadithi inayosema mtu hafai kusema huyu ni mke wangu au huyu ni mume wangu, wakiwa hawajaoana hata kwa mzaha na mtu kusema mimi si muislamu yafaa asilimu.

SWALI:


Swali kutoka Somalia, kwa Saida Abdul kadir


Je ipo hadithi inayosema mtu hafai kusema huyu ni mke wangu au huyu ni mume wangu, wakiwa hawajaoana hata kwa mzaha na mtu kusema mimi si muislamu yafaa asilimu.


JAWABU:


Katika mambo ambayo yatakiwa watu kutoyachukulia mzaha ni kuyatumia maneno ya kidni na kisheria katika sehemu isokuwa zake na kuleta matatizokwa mtu akiwa anjua au hajui. Allah mtukufu ametutakataza kwa kutaja hali za wanafiki waulizwapo kuhusu maneno yao:

وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ قُلْ أَبِاللَّهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنْتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ (65)

“Na ukiwauliza, wanasema: Sisi tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Mlikuwa mkimfanyia maskhara Mwenyezi Mungu na Ishara zake na Mtume wake?” Tawba: 65
Na Allah mtukufu akaweka wazi kuwa maneno hayo yakiwa yanapelekea ukafiri basi watakuwa wamekufuru bila kujali neno lao kuwa ilikuwa ni utani na mchezo akasema:
“Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu.” Tauba:66
Na wala haisemwi kuwa walikuwa wanafiki ndani ya nafsi zao kwa hivyo haiwi sawa kuileta hukmu hiyo kwa wenye kusema bila ya unafiqi, kwani Allah mtukufu anatutakaza kutumia lafdhi mbaya zenye tafsiri ya ukafiri hata kama ni zetu ni njema, alipowakataza waislamu kwa kusema :

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انْظُرْنَا وَاسْمَعُوا وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ (104)

“Enyi mlio amini! Msiseme: "Raa'ina", na semeni: "Ndhurna". Na sikieni! Na makafiri watapata adhabu chungu” Baqarah:104
Na yalikuja makatazo hayo kwa kuwa ni neno ((rainaa)) walikuwa wakilitumia wasiokuwa waislamu kumfanyia istihzai Mtume s.a.w. kwa lugha ya kiebrania lakini kwa Kiarabu lina maana sawa na neno la pili ((undhurnaa)) waliloambiwa watumie, yote hayo ni kuondosha kujifananisha na makafiri na kutotumia maneno yenye utata wa kimaana ndani yake.
Na Muislamu daima anaweka katika akili yake katika lafdhi na maneno ayatoayo kwani atahesabiwa kwayo, Amesema Allah mtukufu:

مَا يَلْفِظُ مِنْ قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ (18)

“Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.” Qaaf : 18
Na yamekuja makatazo khasa katika kutumia lafdhi za ndoa, talaka, kumrejea mke, na kumuachia huru mtumwa, amesema Mtume s.a.w.


"ثَلاثٌ جِدُّهُنَّ جِدٌّ ، وَهَزْلُهُنَّ جِدٌ : الطَّلاقُ ، وَالنِّكِاحُ والرُّجْعَةُ"

“Mambo matatu, ukweli wake ni kweli na utani wake ni kweli, talaka, ndoa na kumrejea mke” kaipokea Abi Dawud 2194, Tirmidhi 1184, Ibn Maja 2048.
Nayo ina Daraja ya Hassan, kwa Muhadddith wa zama zetu Sheikh Saeed Bin Mabrouk Alqannubi – Allah mtukufu amuhifadhi -.
Kama ambavyo haijifichi ndani yake kuwa kuna uongo katika qauli hiyo, nayo si katika tabia za waislamu wala si katika mwenendo wa Mtume S.A.W. kwani yeye alikuwa akitaniana lakini akisema kweli katika utani wake.
Hivyo muislamu ajiepushe na yale yatakayomuweka katika makosa, na ikiwa jambo limekubainikia ukweli wake lifuate, na lilokubainikia liwache, lenye utata usiliingie na kulisemea bora kukaa kimya na kufanya yaliyothibiti kwa usalama wa dini, dunia na akhera yetu.


Wassalaamu alaykum warahmatullah wabarakatuh.


Khamis bin Yahya Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment