Ibadhi.com

34: JE ni vizuri kisheria kusali Salat dhuhur pekee yake kwa wakati wake na Alasar peke yake kwa wakati wake AU kuzichanganya rakaa mbili za dhuhur na rakaa mbili za asar(Qaras) kabliya au taakhir ?

SWALI:

Asalam alaikum.
mimi ninapofanyakazi na ninapoishi ni masafa yanayoruhusiwa kusali safar.salaa ya adhuhuri inanikuta kazini na salaa ya Alasar vile vile inanikuta kazini.JE ni vizuri kisheria kusali Salat dhuhur pekee yake kwa wakati wake na Alasar peke yake kwa wakati wake AU kuzichanganya rakaa mbili za dhuhur na rakaa mbili za asar(Qaras) kabliya au taakhir ?

JAWABU:


Sala zilifaradhishwa rakaa mbili mbili kwanza wakati wa Makka, kabla ya Mtume s.a.w. kwenda Israa na Miiraj.
Amepokea Bii Aisha R.A.


" Sala za faradhi zilifaridhishwa rakaa mbili mbili, kisha zikazidshwa rakaa mbili kwa wakazi na kubakishwa mbili mbili kwa wasafiri" ispokuwa maghribi yenyewe ni rakaa tatu bila kupunguwa.
Hivyo katika sala hii kuna mas ala mawili :

1. KUPUNGUKA RAKAA KWA MSAFIRI.

Ikiwa msafiri anasali peke yake au anasalisha basi inamlazimikia kusali sala zote za rakaa nne kwa rakaa mbili tu. Na ikiwa ataisali kwa rakaa nne sala yake itakuwa imeharibika.

Amma akisali nyuma ya Imam Mkazi (ambaye si msafiri), basi inamlazimu kusali rakaa zote nne, na kuingia katika sala kwa nia ya kusali kwa mujibu wa rakaa za Imam mkazi.

2. KUCHANGANYA SALA MBILI PAMOJA

Hili limewekwa kwa yule aliye katika mwendo na kuwa hawezi kuipata kila sala kwa wakti wake kutokana na dhurufu za safari, sio kwa vingine.

Naye halazimishwi katika hili, bali ni khiyari kwake. Amma aliye katika hali ya utulivu anaambiwa asali kila sala kwa wakati wake, kwa jamaa msikitini.

Hivyo Jawabu ya swali lako:
KASALI NA JAMAA MSIKITINI KILA SALA KWA WAKATI WAKE, BILA KUZICHANGANYA.

Wallahu Aalam.

Abu Muslim Khamis Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment