Ibadhi.com

5. JE, KUSOMA KHITMA BAADA YA KUFIWA NI SUNNA AU FARDHI?

Ndugu yetu Said Moh'd Abdallah Al Harthy kutoka Oman anauliza

Swali:

Je, kusoma khitma baada ya kufiwa na mzazi wako,ndugu yako au mwanao ni suna kiislam au fardhi?

JAWABU:

Kusoma Khitima baada ya kufiwa na mzazi au ndugu au mwana au yoyote katika jamaa, hilo si katika Sunna wala si Fardhi, hilo la Khitima ni jambo walilolipitisha baadhi ya watu tu na likazoeleka katika jamii kwa muda mrefu.

Kwa hiyo hilo si Sunna wala Faradhi.

Basi mwenye kutaka kumfanyia wema maiti wake, anatakiwa apite mlango wa sadaka, au kumuombea dua ya pekee si dua ya kukusanyika.

Imekuja katika athari za Mtume wetu (s.a.w) kuwa alikuwa akichinja na kugawa sadaka ya kichinjwa hicho kwa ajili ya Mama wa Waumini Bibi Khadija bint Khuweilid (r.a) mke wake (s.a.w) wa mwanzo.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment