Published By Said Al Habsy  SWALI
Tunaomba kauli sahihi kuhusu Muisilaamu kumuoa mwanamke mkristo.
السؤال: نسأل عن القول الصحيح في زواج المسلم بامرأة نصرانية. JAWABU الجواب
➡Muisilamu anatakiwa kuoa mwanamke Muisilaamu mwenzake, kwa kuwa huyo ndie analingana nae katika sifa ya Dini.
المسلم يطلب منه الزواج بمسلمة، لتكافئهما في صفة الدين.
➡Na zimekuja dalili nyingi za kisheria kuonyesha umuhimu wa kuchagua mwenye Dini na tabia njema katika ndoa.
وقد وردت أدلة كثيرة في بيان أهمية اختيار ذات الدين والخلق الحسن في الزواج.
➡Wakrsto katika zama hizi wamekwenda kinyume na Dini na Itiqaadi sahihi ambazo zilikuwa katika vitabu walivyo kuja navyo Manabii walio tangulia.
النصارى في هذا العصر قد حادوا عن طريق الحق في الدين والعقيدة التي كانت في الكتب التي جاء بها الأنبياء السابقون.
➡Na ile sifa ya kuwa wao ni watu wa kitaabu haipo tena kwao, na wala haifai kuwaoa kabisa, hata aseme mwenye kusema kufaa kuwao watu hao.
ووصفهم بأنهم أهل الكتاب لا وجود له فيهم، ولا يحل نكاحهم وإن قال من قال في جواز ذلك فيهم.
➡Qurani tukufu ndio marejeo yetu katika kujua haki na batili katika mambo yote.
القرآن الكريم هو المرجع في معرفة الحق والباطل في الأمور كلها.
➡Amesema Allaah sw: (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنْكُمْ ۖ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا) [Surat An-Nisa 59]
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.
➡Tazama aya zifuatazo kuhusu watu wa kitabu , tena katika zama za nyuma zaidi ambapo vitabu vyao ndio vilikuwa vimeanza kuharibiwa:
تأمل الآيات التالية عن أهل الكتاب، وهذا كان في الزمن السابق الذي كان تحريف كتبهم في مطلعه:
1- (قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ ۚ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ) [Surat Aal-E-Imran 64]
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.
2- (مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَٰكِنْ كَانَ حَنِيفًا مُسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ) [Surat Aal-E-Imran 67]
Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.
3- (يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَأَنْتُمْ تَشْهَدُونَ) [Surat Aal-E-Imran 70]
Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu ilhali nyinyi mnashuhudia?
4- (يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ) [Surat Aal-E-Imran 71]
Enyi Watu wa Kitabu! Mbona kweli mnaivisha uwongo, na kweli mnaificha na hali mnajua?
5- (وَقَالَتِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَىٰ نَحْنُ أَبْنَاءُ اللَّهِ وَأَحِبَّاؤُهُ ۚ قُلْ فَلِمَ يُعَذِّبُكُمْ بِذُنُوبِكُمْ ۖ بَلْ أَنْتُمْ بَشَرٌ مِمَّنْ خَلَقَ ۚ يَغْفِرُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَنْ يَشَاءُ ۚ وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ) [Surat Al-Maeda 18]
Na Mayahudi na Wakristo wanasema: Sisi ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake. Sema: Basi kwa nini anakuadhibuni kwa ajili ya dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu tu kama wale wengine alio waumba. Humsamehe amtakaye na humuadhibu amtakaye. Na ni wa Mwenyezi Mungu tu ufalme wa mbingu na ardhi. Na marejeo ni kwake Yeye.
6- (يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ عَلَىٰ فَتْرَةٍ مِنَ الرُّسُلِ أَنْ تَقُولُوا مَا جَاءَنَا مِنْ بَشِيرٍ وَلَا نَذِيرٍ ۖ فَقَدْ جَاءَكُمْ بَشِيرٌ وَنَذِيرٌ ۗ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ) [Surat Al-Maeda 19]
Enyi Watu wa Kitabu! Bila ya shaka amekujilieni Mtume wetu akikubainishieni katika wakati usio kuwa na Mitume, msije mkasema: Hakufika kwetu mbashiri wala mwonyaji. Basi amekujieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu anao uweza wa kila kitu.
7- (لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنْصَارٍ) [Surat Al-Maeda 72]
Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.
8- لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَٰهٍ إِلَّا إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِنْ لَمْ يَنْتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru.
[Surat Al-Maeda 73]
➡Aya za kitabu cha Allaah sw ziko wazi kuonyesha kuwa hawa watu hawana sifa ya kuwa ni watu wa kitabu.
آيات كتاب الله تعالى واضحة في بيان أن هؤلاء القوم ليس فيهم وصف كونهم من أهل الكتاب.
➡Hawa Watu wanaitikadi kuwa kuna: mungu Baba , mungu mwana na kadhaa na kadhaa, kisha anatoa fatwa Muisilaamu kuwa inafaa kuwaoa watu wa aina hii??!!
هؤلاء القوم يعتقدون أن هناك: الإله الأب، والإله الابن، وكذا وكذا، ثم يفتي من يفتي بجواز زواج مثل هؤلاء؟؟!!
➡Amma kutumia hoja ya kufaa kuwaoa watu wa kitabu kwa aya ufuatayo:
أما الاحتجاج باﻵية التي الزواج بهؤلاء في الآية التالية:
(الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَنْ يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ) [Surat Al-Maeda 5]
Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a'mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.
➡Naam; aya hiyo inaonyesha kuwaoa watu wa kitabu wenye sifa za kiumini zilizotajwa katika Qurani tukufu.
نعم تلك اﻵية تبيح الزواج بأهل الكتاب ، الذين لهم تلك الصفات الإيمانية التي ذكرت في القرآن الكريم.
➡Na watu hao katika zama hizi hakuna , wote wamekuwa wanaingia katika kundi la washirikina - ila wale aliowarehemu Rabb - kwa sababu nyingi sana, miongoni mwazo ni:
وهؤلاء بتلك الأوصاف غير موجودين ، فكلهم يدخلون تحت وصف المشركين، - إلا من رحم ربي - لعدة أسباب؛ منها:
1- Kuitakidi kuwa Mungu ana sifa ya utatu.
اعتقادهم أن الله ثالث ثلاثة.
2- Kuitakidi kuwa Isa bin maryam ni Mtoto wa mungu au yeye mwenyewe ndie mungu.
اعتقادهم أن عيسى بن مريم ابن الله ، أو هو بنفسه إله.
3- Kuitakidi kuwa Nabii Isa alisulubiwa katika msalaba na kuuliwa.
اعتقادهم أن عيسى بن مريم صلب ومات على الصليب.
4- Kuikanusha Qurani tukufu na aya zake.
إنكارهم القرآن الكريم وآياته.
5- Kuacha kumfuata Mtume Muhammad s.a.w katika Imani na Sheria za kiisilaamu.
ترك اتباعهم نبينا محمد صلى الله عليه وسلم، في اﻹيمان والشريعة الإسلامية.
➡Haya ni baadhi ya machache katika mengi juu ya suala hili, na wala fatwa ya kujuzu kuwaoa hawa watu haina maana yoyote katika mizani ya sheria.
هذا قليل من بين كثير عن هذه المسألة، والفتوى بجواز الزواج بهؤلاء لا اعتبار له في ميزان الشرع.
➡Na kuna baadhi ya waisiilaamu wameshapoteza watoto wao kwa sababu ya ndoa chafu za aina hii, wamekuwa na watoto wenye dini tofauti; Baadhi yao wanakwenda msikitini, na wengine wanakwenda kanisani.
وهناك بعض المسلمين قد ضيعوا أبنائهم بسبب مثل هذا الزواج الشنيع،صاروا هم وأبناؤهم مختلفين في الديانة؛ بعضهم يذهبون إلى المساجد وبعضهم إلى الكنائس.
➡Tahadhari sana muisilaamu kuwafanya mayahudi na manasara kuwa vipenzi vyako, kuna kupoteza dini katika hilo.
احذر أيها المسلم من اتخاذ اليهود والنصارى أولياء، فإن فيه إضاعة الدين.
➡Amesema Allaah sw: (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ) [Surat Al-Maeda 51]
Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
➡Namuomba Allaah sw atunusuru na kufuata mila potofu, na fatwa zenye kwenda kinyume na Kitabu na Sunna.
أسأل الله تعالى أن ينصرنا من اتباع الملل الباطلة، واتباع الفتاوى الضالة المخالفة للكتاب والسنة.
ALLAAHU AALAM الله أعلم
➡Jawabu kutoka kwa SH. SHAABAN AL BATTAASHY. |