Print this page

016: Naomba unitajiye watu ambao wanaolazimika kulipa na kutowa kaffara "❓

Written by

SWALI:

Shekh , " Naomba unitajiye watu ambao wanaolazimika kulipa na kutowa kaffara "❓

JAWABU. 

بِسْم الله الرحمن الرحيم

Naam❗.

- Watu ambao watakaopaswa kulipa na kutowa kaffara ni :-

 1. Mpuzaji wakutokulipa ramadhani iliyopita bila sababu.

Hukmu yake :-
Mtu Kama huyu ambaye imeingia ramadhani nyengine bila kulipa deni la nyuma hukmu yake ni:-

Atatubia kwa kupuuza kwake wajibu wa kufunga

- atalipa funga alizoziacha zoote.

- atalisha kila siku maskini siku aliyeipoteza.

2 - Mwenye kuasi na kuvuka mipaka.

- mwenye kuasi hapa amekusudiwa Yule ambaye aliyekwenda kinyume na sheria za funga au akavunja nguzo au shart la funga❗

- Kwa mfano :-

❗Mwenye kula au kunywa maksudi.

❗Mwenye kufanya tendo la ndowa mchana.

❗ Mwenye kujitowa Nanii kwa njia yoyote ile .

Hukmu Yao :-
- Kutubia na kuomba msamaha.

- Kulipa funga ya siku hio aliyofanya kosa hilo.

- Atatowa kafara nzito (kaffara mughaladha) nayo ni hivi :-

Kuacha mtumwa huru, kama hakumpata basi atafunga miezi 2 mfufulizo. 

Kama ha kuweza basi..

- Atalisha maskini 60
..
والله أعلم

Read 2530 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba