Print this page

0015: Naomba unitajiye watu ambao wanaolazimika kula na kulisha maskini ❗ ❓

Written by

SWALI.

Shekh, " naomba unitajiye watu ambao wanaolazimika kula na kulisha maskini ❗"


JAWABU.


بِسْم الله الرحمن الرحيم


- Watu ambao wanao lazimika kula mchana na Kisha kulipa ni :-


- Mgonjwa ambae ugonjwa wake ni wenye kuendelea -  yaani mgonjwa ambaye hawezi kabisa kufunga wala hakuna matarajio ya kupona ugonjwa wake ❗

- Mtu mzima sanaa - Amekusudiwa hapa ni babu ambaye ni mtu mzima sanaa na hajiwezi au Bibi ambaye ni mtu mzima Sanaa na hajiwezi ..

Hukmu ya watu hawa wawili :-

- Watalazimika kula mchana na kulisha kila siku nusu pishi au watamlisha kila siku maskini mmoja kwa mlo mmoja basi ( mlo wa mchana)

- Dalili yake
Fungua Surat baqarah aya 184 ...

" وعلى الذين يطيقونه فدية طعام مسكين "

Neno "" يطيقونه"
Ibni Abaasi r.a amelitafsiri kuwa "" wanapata shida na dhiki ""

- Maana ya aya :-
" Nawale wanaopata shida ( ktk kufunga huko) basi watatowa fidya ya kulisha maskini "

- Qauli hii ndio yenye kutegemewa ktk fatwa za mashekhe wawili watukufu ( Shekh Khalili na Sheikh Qannubi) Allah awahifadhi ..

Tanbihaat

- Hukmu ya kupewa wao (Hao wawili mgonjwa wenye kudumu na mtu mzima) ni vile kuenekana kwao na aghlab ya dhanna ,
Lakini watakapopata na afya njema siku za usoni hukmu hio itaondoka .

- Utaratibu au jinsi ya kutowa fidya ni hivi Kama ifuatavo ;:-

Unaweza kumlisha maskini mmoja Tu huyo huyo kwa kila siku 29 au 30.

Na vile inajuzu kwako kulisha maskini 29 au 30 kwa mpigo.

Huwezi kulisha maskini kabla ya ramadhani kuingia, asli ni kumlisha kwa kumpa chakula lakini hakuna tatizo kama ukampa thamani yaani pesa ikiwa hakuna wa kuku ali chakula.

Nusu pishi imeqadiriwa kuwa ni kilo mmoja na gram 20 na atakae ongeza zaid ya hapo Allah atamuongezea .

والله أعلم

Read 3030 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba