Print this page

0014: Nakuomba unitajie shuruti za funga❗❓

Written by

SWALI:

Shekh :- Nakuomba unitajie shuruti za funga❗❓

JAWABU:

Ibada yoyote bila kutambuwa masharti yake huwezi kuifanya kiusahihi daima utakuwa wadapiya gari tu bila kujuwa wapi unakwenda..

Na leo biidhnilaah tutamalizia na sharti la pili :-

2 - KUJIZUIYA NA VIFUTURUSHAJ TANGU KUCHOMOZA KWA AlFAJIRI MPAKA KUZAMA KWA JUA KWA NIA

-Kujizuiya na vifuturishaji ambazo vinaharibu funga yako

Navo viko aina 4 kuu

1 - kuingiza kitu kutoka njee kuiingia ndani

Kama vile kuingiza chakula au kinywaji au kupitia ktk tundu za macho au mdomo au kupigwa sindano yenye chakula.

2 - Kutowa kitu kutoka ndani kwenda injee.

Kama matapishi kwa maksudi au kujitowa manii.

3 - Tendo la ndowa mchana wa ramadhani.

4 -Kutenda maasi

Kama vile kusengenya, kusema uongo na mfano wake .

Amesema mtume wetu s.aw. " ولا صوم إلا بالكف عن محارم الله "

" wala hakuna funga mpaka ujizuiye na Yale aliyeyaharamisha Allah "

Tangu kuchomoza kwa juwa mpaka kuzama :-

- na hii ili tuwe mbali na mayahudi na manasara Kwani wao wanafunga baada ya sala ya isha .

- Sisi Allah katutaka tufunge tangu juwa la kweli lachomoza (kabla ya adhana ya pili )

Allah anasema ktk Surat baqarah aya 187

" وكُلُوا واشربوا حتى يتبين لكم الخيط الأبيض من الخيط الأسود من الفجر "

" kuleni na kunyweni mpaka ikubainikien kwenu uweupe wa alfajiri ktk weusi wa usiku "

Pamoja na kutia nia.
Naam ibada yoyote ile inasimamiwa na nia kabla yake.

Amesema mtume wetu s.aw. :-

"إنما الاعمال بالنيات "

" hakika ya matendo hutanguliwa na nia "

والله أعلم

Read 2610 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba