Print this page

012: Naomba ufafanuzi wa "Muandamo wa mwezi wa ramadhani " ❓

Written by

SWALI:

shekh, " naomba ufafanuzi wa "Muandamo wa mwezi wa ramadhani"

JAWABU:

Naam!..
- tuelewe kuwa "kufunga na kula "kunaambatana moja kwa moja na kuonekana kwa mwezi Mtume wetu s.a.w. Ametuelekeza nini tufanye anasema:

"  صموا لرؤيته وأفطروا لرؤيته "..
"Fungeni kwa kuona kwake huo ( mwezi) na kuleni kwa kuonekana kwake huo( mwezi).
Na hadithi zimekuja kwa njia tofauti na matamshi mingi lkn yoote yanalenga kuwa tuuwangalie mwezi ktk Hali mbili hizi..

- na kuonekana kwa mwezi kunatafautiana kwa mujibu ya utafauti wa miji yetu ktk kuchomoza kwa juwa na kuzama kwake..

Kutokana na namantiqi hio huwezi kabisa kulinganisha kuonekana pahala flani ikaweza kuathiri mji mwengine wa mbali .kama vile ibada ya sala
Sala ya adhuhuri inathibiti kwa kutenguka kidogo juwa au sala ya maghrib inaingia na kuthibiti kwa kuzama kwa juwa lote.
Kwa hivyo huwezi kulinganisha kabisa ukasema kuwa ikiingia adhuhuri zanzibari kwa mfano ndio walioko marekanani au india au suidia na wao wasali sala ya adhuhuri !! 
Hii haingii akilini kabisa kwani wao wanamuda wao wa machomozo ya juwa na kuzama kwake ..
Pesa ya oman huwezi kabisa ukaitumia vile vile ilivo ukanunuwa nazi soko la Chake pemba lazima utaichenji kwanza ndio uitumie kwa pesa iliyopo pale tanzania.

-  na madai ya baadhi ya watu kusema kuwa nchi flani kwa mfano suudia ndio inafuatwa kwa vile inazingatiwa ndio chimbuko la uislamu pindi ukionekana mwezi suudia ndio dunia nzima wafunge madai haya sio sahihi kabisa .
Uislamu unafuatwa popote utakapukuwepo wewe sheria hazikubatanishwa na nchi ya suudia.

Kitu cha kujiiliza sasa ni hichi:-
Wale waliopo katika nchi zao mchana na wale waliopo usiku vp watafunga
Na funga inaanza kwa kuchoma alfajiri na mwisho wake ni kuzama kwa juwa ?

-  dalili tosha ya kuonyesha kuwa kila mji una muandamo wake ni ile hadithi mashhuri kwetu sote. ( hadithi ya kureybu)

Ambapo ABDALLAH ibni abbasi r.a ali ukatakataa kata mwezi aliouona kureyb pindi alipokuwa shamu kikazi na

Kureyb akashaangaa huku akimuiza
" أو ما تكتفي برؤية معاوية وصيامه "
" Jee hutosheki wewe na mwezi aliyouwona muaawiya na kufunga kwake " !!?

Abdallah bin abaas r.a akamjibu :-
" لا هكذا أمرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم "
" laa (sitotosheka na hayo) hivi ndivo alivotuamrisha mtume wetu s.a.w )

Hii hadithi iko wazi kabisa kuwa ibni abaas kaukataa mwezi ulioindama sham na Hali yakuwa madina na shamu ni karibu vip iwe miji ya mbali Sanaa isende Kama alivokwenda abdallah ibni abaas . Na kwanini abdallah ibni abaas r.a asifuate mwezi wa muaawiya??

Na ktk fani za hadithi pindi sahaba akisema
"أمرنا / نهيناعن كذا /كنّا نعمل.
" ametuamrisha /ametukataza na kitu flani/ tulikuwa tukifanya.
Hizi huzingatiwa kuwa hukmu yake ni inapandishwa moja kwa moja kwa mtume s.a.w .

والله أعلم 

Tanbihi muhimu:-
1 - Nas-ala haya kuna khilaafu baina ya ndungu zetu nawawo kwetu wana nia safi kwetu kwa ufahamu wao mwengine wa hizi hoja.

2 - Tofauti zetu hizi isiwe ndio firimbi ya kutangaza uaduwi na chuki na ukhasama baina yetu Bali iwe ni uwanja wa kupeana hoja kwa hoja .

3 - Wako wenzetu -allah atuongoze sisi na wao- wanaufarikisha umma na kutukanana na kudharau wenzao kwa sababu hii Tu ya " kutafautiana kufunga"

4 - Hii isiwe ndio sababu ya kuwa hivo bali tuzidi kupendana na kushikamanana japo tumetafautiana.

والله أعلم

 

Read 3657 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba