Print this page

011: Nitajiwe sababu za kuthibiti kufunga mwezi wa ramadhani ❓

Written by

SWALI:

Shekh :- "nitajiwe sababu za kuthibiti kufunga mwezi wa ramadhani "

- huwezi kujitia kufunga kivyako vyako tu ila kuna sababu moja katika hizo zikikuthibitikia basi hapo sheria inakutaka ufunge sababu wenyewe ni :-

1⃣)- kuonekana kwa mwezi
2⃣)- kuenea kwa khabari.
3⃣)- kukamilisha siku 30 za mwezi wa shaabani.

UFAFANUZI:-

Kuonekana kwamwezi

Imethibiti ktk Surat baqarah aya " فمن شهد منكم الشهر فليصمه "  "atakaeushuhudiya mwezi katiyenu ( na akawepo ktk mji wake) basi na aufunge"
Na ktk hadithi sahihi mtume s.a.w anasema ;-  " لا تصوموا حتى تروا الهلال ولا تفطروا حتى تروه فإن غم عليكم فأكملوا العدة ثلاثين يوما " 
" musifunge mpaka muuone mwezi na musile (skukuu) mpaka muuone huo ( mwezi) , nakama mukizibiwa na mawingu (mukautafuta musiuwonee) basi kamilisheni idadi ya siku 30 za ( shaabani)

Naam!
Dalili hizi ziko wazi kabisa kuwa funga inaambatana na kuonekana kwa mwezi na usichokore chokore ukatafuta mwezi wa nchi nyengine na Hali hadithi mwisho iko wazi kabiza

فإن غم عليكم"   "mukizingwa na mawingu kwenu" hii yaonesha wazi ima tutauona au tusiuwone bila kudapiya miezi ya watu na kama ilivothibiti ktkhadithi ya ibni abaas r.a kuwa amesema mtume s.a.w anasema :-
"" أن لكل قوم هلالهم "  "Kila watu ( wa miji) wana mwezi wao""

Kukamilisha siku 30.

Pindi ikishindikana baada ya kuuwangaliya mwezi vzr na mwisho wa mambo tukaambiwa kuwa mwezi haujaonekana hapo basi utapaswa kukamilisha siku 30 za mwezi wa shaabani usiwe naharaka na kudapiya miezi ya watu. Imethibiti ktk hadithi ya nyuma kwamba "فإن غم عليكم فأكملوا العدة ثلاثين من شعبان"  "Mukizingwa na mawingu basi kamilisheni siku 30 za shaabani"

Kupata khabari.

Haiwezekani ikawa sooooote ndio tumeuona mwezi ... Inaweza kutokezea baada ya muda flani tukapata khabari kwa mtu flani au watu flani kuwa wao wameuona mwezi ktk kijiji flani mudaa kadhaa

Na ktk hili kuna shuruuti ili tumkubali huyo Jamaa aliyeuona mwezi :-nazo ni
1)- mwenye akili
2)- kabaleghe
3)- mwanamme
4)- muaminifu ktk Dini yake
5)- na shahada yake hio isijekuwa kinyume na anayosema.

Imethibiti ktk hadithi sahihi iliyopokewa na ibni abaas r.a kuwa "" alikuja bedwi mmoja huku akisema ewe mjumbe wa allah hakika yangu Mimi nimeuona mwezi mtume s.a.w akamuuliza jee unashihudiya kuwepo kwa Allah kuwa yeye ni mmoja ?? Na mm ni mjumbe wake ?? Akasema ndio
Basi hapo mtume s.a.w akamuamrisha bilaal awatangazie watu kesho wafunge"
Hii kuonesha sababu Kama hii unaweza kuitumia kwa kuthibiti kwa kuingiza kwa mwezi lkn kwa masharti.

والله أعلم

Read 2510 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba