Print this page

010: Nakuomba unimalizie funga za sunna ❓

Written by

SWALI:

Shekh: - nakuomba unimalizie funga za sunna ?

JAWABU:

Naam - Ni muendelezo wa kutaja Sunna za kufunga na tunamaliza kutaja sunna hizo za kufunga.

4 - ( sifa za shawaal)
Funga 6 za shawali ni zile zinazokuja baada ya funga ya ramadhani kumalizika na sikukuu ya kwanza.. Hapa tena unakhiyari kwako kufunga mwanzo wake au katikati au mwishoni .

- Dalili ya kuthibiti funga hii ni :-
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:" من صام رمضان ثم أتبعه ستا من شوال فذالك صيام الدهر "
" atakae funga ramadhani Kisha akafuatiza na kufunga siku 6 za shawaal basi hio nikama kafunga mwaka "

5 - (siku 9 dhiyl-hija)
Funga hii huwa inakuja pindi Tu inapiingia dhul-hija ila siku ya sikuu ni haramu kufunga na Fadhila zake ni kubwa Kama ilivothibiti ktk hadithi sahihi

" ما من أيام العمل الصالح أحب إلى الله فيها من هذه الايام ، قالوا ولا الجهاد في سبيل الله ؟
قال إلا من خرج بنفسه وماله ثم لم يرجع"

" hakuna masiku matendo memo yakawayanapendwa zaid mbele ya allah Kama masiku haya, masahaba wakamuulizA mtume s.a.w hata jihaadi ktk njia ya allah? Mtume s.a.w akasema rabda mtu katoka yeye na nafsi yake na mali yake kisha asirejee tena "

والله أعلم

Read 2539 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba