Print this page

009: Naomba unielezee aina za funga za sunna ❓

Written by

SWALI:

Shekh :- " Naomba unielezee aina za funga za sunna."

JAWABU: 

Naam!.

Kuna funga ambazo zimekuja kutuhimiza na kuturaghibisha na kujipendekesha kwa allah wala hakuna ulazima wa kufunga ila kuna Fadhila kubwa zinapatika kwa mwenye kufunga.
Nazo ni :-

1 )-( ayyamu baydhi)

- funga hii maana yake ni masiku matatatu meupee kwani mwezi wakati huo unakuwa unangaaza zaid nazo ni mwezi 13,14 na 15 kila mwezi wa kiislamu.

- Dalili yake:- kutoka kwa abiy hurayra r.a amesema: " ameniusia alkhaliliyli ( mtume s.a.w) juu ya mambo matatu kufunga siku 3 kila mwezi, na rakaa mbili za dhuhaa na kusali witri kabla sijalala "

Na funga hii fadhila zake Kama umefunga mwezi mzimaa.

2 - ( A'shuraa)
-funga hii asili yake ilikuwa mayahudi ndio walikuwa wakiifunga wakati wa jaahiliya alipokwenda mtume wetu s.a.w Madina akawamrisha masahaba wake waifunge funga hii .

- na utaratibu wa kufunga hii kiusahihi zaid kuwa mayahudi wao walikuwa wakiifunga mwezi 9 mtume s.a.w akaturisha tuwakhaalifu ( twende nao kinyuma) yaani tufunge siku moja kabla ya 9 yaani tufunge 8na 9. Au tufunge siku moja mbele yake yaani 9na 10 ili tuonyeshe kuwa sisi tumetafautiana nao.

- Dalili ya maneno hayo ni aliposema mtume wetu s.a.w  " صوموا يوم عاشوراء وخالفوا اليهود وصوموا يوما قبله أو يوما بعده "
" fungeni siku ya a'shuraa ,na kuwenikinyume nao ,na fungeni siku moja kabla ya hio funga Yao ( mwezi 9) au fungeni siku moja baada ya funga Yao " 

- fadhila zake
Amesema mtume wetu s.a.w kuwa
"من صام عاشوراء كان كفارة لستين شهرا وعتق عشر رقبات مؤمنات من ولد إسماعيل"
" atakae funga ya A'shuraa itakuwa ndio kafara yake (ya kufutiwa madhambi ) yake miezi 60 na kama kawaacha huru watumwa waumini kumi ktk kizazi cha nabii ismaili a.s""

3 - ( Arafa)

-  Siku ya Afara ni nguzo kubwa ambayo mahujaaj woote wanamiminika ktk mlima huo wa arafa.

-  Na funga ya arafa ambyo ni mwezi 9 imethibiti uhakika wa funga hio kwa wale tu walikuwa hawapo ktk Kiwanja hicho Ama kwa mahujaaj sio vzr kufunga siku hio kwa vile watadhaufika ktk ibada zao
Na ktk hili kuna khilaafu.

- Fadhila ya funga hii kuwa imethibiti dalili sahihi kuwa mtume s.a.w anasema:-
" صوم يوم عرفة كفارة سنتين."
" funga ya siku ya arafa ni kafara( ya kusamehewa) miaka mwili( mmoja uliopita na wapili ujao)"

Tanbihi muhimu

Siku ya Arafa Kama ilivothibiti kuwa ni mwezi 9 na sisi tunafunga kwaajili ya kupata fadhila hizo inshaallah ..hatufungi kwasababu wao mahujaj ndio siku ile wamesimama kwasababu tarehe za miandamo zinatafautiana wako wengine siku hio kwao ni mwezi 8 kwa mujibu wa muandamo wao, kwa hivyo wao watapaswa waifunge siku ya pili yake.

Na wako wengine wakati huo mahujaaj wamesimama wao ni usiku vp watafunga??na hakuna funga usiku kwa hivyo moja kwa moja kila nchi itaangalia kwa mujibu wa muandamo wake Kama vile ungiaji wa sala na kutoka kila mji unawakati wake Allah anasema ktk Surat baqarah aya 189

" يسؤلونك عن الأهلة قل هي مواقيت للناس والحج"
"Wanakuuliza kuhusu miezi ( mabadiliko yake ) sema hio ndio nyakati za watu na ( nyakati) za hija"

- Na ktk hili kuna khilaafu kwa wenzetu na isiwe ndio uwanja wa kudharauliyana na kukufurishana na kutuhimiyana baina yetu.. Bali iwe ni uwanja wa kuelimishana kihoja tu.

والله أعلم

Read 4643 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba