Print this page

007: Naomba unielezee aina za funga za ulazima ❓

Written by

SWALI:

Sheikh - Naomba unielezee aina za funga za ulazima ❓ 

JAWABU:

- Funga ziko aina nyingi kwa kuja kwa matokeo tofauti na huja kwa hukmu tofouti. Nazo ni kama hizi:~

1⃣ - ("funga ya nadhiri")

Hii ni ile anayojilazima binaadamu mwenyewe,

Kwa mfano atakaposema :- " Naweka nadhiri nikifanikiwa kupata kitu flani basi nitafunga mwezi au mwezi flani"

- Hukmu ya nadhiri hii kuwa atalazimika kuitekeleza funga hii

- Dalili yake :-

Imethibiti kuwa mwanamke alisema kumwambia mtume wetu S.A.W. :~

" Ewe mjumbe wa allah hakika ya mama yangu kafa na anadaiwa funga ya nadhiri, je nimfungie❓

Mtume S.A.W. akasema:~ " Je waonaje ingekuwa mama yako anadeni si ungelilipa lile deni lake❓

Akasema Yule mwanamke " ndio " basi mtume S.A.W. akamwambia aifunge saumu ile (ya nadhiri).

2 - ( funga ya tamatui)

Funga hii ni kwa Yule aliye fanya kuinganisha Hija yake na umra kisha asiweze kutekeleza ibada ya kuchinja mtu huyu atapaswa kufunga siku 10; 3 atazifunga akiwa ktk ibada ya Hija na 7 atazifunga pindi akirudi nyumbani kwake.

- Dalili yake, Allah Anasema katika Surat Baqarah, Aya 196.

" فصيام ثلاثة أيام في الحج وسبعة إذا رجعتم "   Atafunga siku 3 akiwa katika ibada za hija na 7 atazifunga atakaporudi (nyumbani)

3 - (Funga ya kafara)

Hii ni funga ya kulipa kafara pindi ikitokezea kauwa au kumsema mkewe ( kuwa Kama mgongo wa mama yangu, dhihaari) au kafara ya kuaapa kisha asitekeleze kiapo chake .

Na hii huja baada ya kushindikana kutekeleza kuacha mtumwa huru.

Allah Anasema katika Surat An - Nisaai, Aya 92, katika kafara ya kuuwa kwa bahati mbaya tu.

" فمن لم يجد فصيام شهرين متتابعين توبة من الله "

Na katika kafara ya kumrejea mke baada ya kumwita (dhihaar), kama mgongo wa mama yangu, katika Surat Mujaadala, Aya ya 4

" فمن لم يجد فصيام شهرين متتابعين من قبل أن يتماسا "

"Basi asiyeweza kuacha huru mtumwa basi atapaswa kufunga miezi 2 mfufulizo kabla ya kumgusa (kumuingilia mkewe)

Kwa ufupi 

- Funga za ulazima ni funga ya Ramadhani, funga ya kuweka nadhiri, funga ya kutowa kafara na funga ya tamatui.

و الله اعلم

 

Read 4828 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba