Print this page

006: Naomba nitajiwe Fadhila za funga Ramadhan ❓

Written by

SWALI:

Sheikh :- Mimi nauliza hivi.. ❓ " Naomba nitajiwe Fadhila za funga Ramadhan ❗

JAWABU: 

✏️ Funga ya Ramadhani Ina fadhila kubwa sanaa jinsi ya utukufu wake na cheo chake.

Mtume wetu S.A.W. Amesema :-

" Lau mungekuwa munajuwa fadhila na utukufu uliopo katika mwezi huu basi mungetamani Ramadhini iwe mwaka "

- Na Allah kausifu mwezi huu kuwa ndani yake kumeteremshwa Qur-an na katika usiku wa laylatu qadri ambao ni bora kuliko miezi 1000 . Allah anasema ktk Surat Qadri, Aya ya 1

" إنَّا أنزلناه في ليلة القدر " ..

"Halika ya sisi tume iteremsha (hio Qur-an) katika usiku wenye cheo kikubwa"..

- Funga na Qur-an zitakuja siku ya qiyama ili kumuombea aliyefunga na kuisoma Qur-an.

Imethibiti hadithi sahihi ambayo kaipokea Abdillah bin Amri kuwa Mtume S.A.W.

قال
 "الصيام والقران يشفعان للعبد يقول الصيام : أي رب منعته الطعام والشهوات بالنهار فشفعني فيه، ويقول القران :
⭐ منعته النوم بالليل فشفعني فيه فيشفعان"

" Funga na Qur-an zitamuombea (siku ya qiyama) mja, funga itasema kumuambia mola wake:

Hakika yangu nimemzuiya na kula na matamanio wakati wa mchana basi namuombea kwa hilo,

Na Qur-an nayo itasema:

Nimemnyima usingizi usiku basi namuombea kwa Hilo .. Hapo basi ataombewa ( atakubaliwa uombezi huo).

Na katika pepo kuna mlango maalum wa waliofunga unaitwa "Rayyan"

Kama ilivothibiti katika hadithi sahihi ambayo kaipokea Suhayl bin Saad:

" في الجنة ثمانية أبواب ، منها باب يسمى الريان لا يدخله إلا الصائمون "

" katika pepo kuna milango minane , katika hio minane kuna mlango mmoja unaitwa Rayyan ambao hawataingia humo ila waliofunga ( lillaah taalaa)

- Na mfungaji aliyekuwa na iman na kutaraji malipo yake basi Allah Taalaa Atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia nyuma.

Imethibiti hadithi sahihi kutoka kwa abuu huraira r.a kuwa mtume S.A.W. amesema:-

" من صام رمضان إيمانا واحتسابا غفر ما تقدم من ذنبه "

" Atakae funga Ramadhani kwa Imani safi (mbele ya Allah) na kutaraji kwake malipo basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia "

- Na mwezi huu unapoingia tu basi kwanza milango ya moto hufungwa na ikafunguliwa ya peponi na mashetani wakadhibitiwa kwa Kutiwa mbaroni ( vitimbi vyao )

Imethibiti hadithi sahihi ambayo kaipokea Abuu Hurayra R.A. kuwa Mtume wetu S.A.W. Amesema :-

" إذا دخل رمضان فتحت أبواب الجنة وغلّقت أبواب جهنم وسلسلت الشياطين "

"Unapoingia mwezi wa Ramadhani basi milango ya pepo hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na wakapigwa minyororo mashetani"

Naam ❗ Hizi ni miongoni tu za Fadhila za mwezi wa Ramadhani .

Allah atufikishe salama na kuifunga Ramadhan kwa iman na matarajio.

Amin yaa Rabiynaa..

والله أعلم 

Read 2950 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba