Print this page

005: Mimi nauliza hivi ni nini hikma ya kufaradhishwa funga ❓

Written by

SWALI:

Sheikh mimi nauliza hivi ni nini hikma ya kufaradhishwa funga ❓

JAWABU 

- Bila Shaka funga ni ibada pekee yenye siri kubwa baina ya mja na mola wake, hebu njooni tuziangalie hizo hekma na utukufu wa kufunga.

1 - Kuitakasa nafsi na kuipa khofu na ulinzi mbele ya mola wake ili apate kuwa mcha mungu ..

Allahu Anasema katika Kitabu Chake kitukufu Surat Baqarah, Aya 183.

". لعلكم تتقون "

" Ili tuweze kumuogopa Allah (kumcha Allah)."

2 - Funga ni Kinga ya maradhi na maovu ..

Naam❗ Funga iliyo kamilika Inamlinda na maradhi mbali mbali katika mwili wake na maradhi ya nafsi yake.

Amesema mtume wetu S.A.W. kuwa:

"" Yoyote yule Kama hakuacha kusema uongo basi Allah hana haja na kujihangaisha kwake na kukaa bila ya kula na kunywa ""

3 - Ni nusu ya subra ..

Naam funga iliyokuwa kuwa sahihi Inakujenga kuwa nasubra kama vile

- Kujizuiya na kula na kunywa na hata kukutana na mke wako wa halali.

- Kujizuiya na maovu na machafu kama, (uongo, kusengenya, kujibizana na maneno maaovu).

Amesema mtume wetu S.A.W.

 "الصِّيَام نصف الصبر" "Funga ni nusu ya subra "

4 - Funga ni Chuo pekee cha kuhurumiana, kusaidiana , kusamehana baina yetu ..

Naam ❗

Katika mwezi huu jinsi ya utukufu wake ni fursa ya pekee kwa waliokhasimiana kukaa wakasuluhisha na kusamehana yaliyopita na ni fursa vile vile ya kuwasaidia kihali na mali maskini na mafakiri..ili nawao wajisikie kuwa na furaha na upendo mbele ya wenzao wenye uwezo..

5⃣ - Funga ina kufundisha uwe Mwenye nidhaamu na kuwa sawa na wenzako ..

 - Ukiangalia wakati wa kufunga na kula ikiwa nchi ziko sawa pamoja katika ufungaji na kula basi utawaona woote wanakula na kufunga kwa muda maalum ..

- woote wanafunga mwezi wa Ramadhani kwa kuona mwezi na kula siku kuu kwa kuona mwezi...

- wooote wanaanza kufunga kwa kuanza alfajiri ya kweli na wanakula kwa kuzama kwa jua.

Hizi ndizo nidhamu za funga hii.

والله أعلم 

Read 2914 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba