Print this page

004: Naomba unielezee funga imefaradhishwa lini❓

Written by

SWALI:

Sheikh :- Naomba unielezee funga imefaradhishwa lini❓

JAWABU: 

- Funga imefaradhishwa mwaka 2 baada ya kuhama Mtume wetu S.A.W. kutoka Makka kwenda Madinat Munawwara na baada ya kubadilishwa kibla kuelekea Al-Qabas.

- Na ilikuwa kufaradhishwa huko ni haramu kukutana kindoa na mkeo usiku wa Ramadhani.

Kisha hukmu hii ikafutwa pale Allah aliposema katika Surat Baqarah, Aya 187

" أحل لكم ليلة الصيام الرفث إلى نساءكم هن لباس لكم وأنتم لباس لهن"

" Mumehalalishiwa kwenu usiku wa funga (ya Ramadhani au nyengineo) kuingiliana na wake zenu kwani wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao."

- Kufaradhishwa funga hii ni siku 30 au 29 nazo Allah amezitaje kuwa ni zenye kuhisabika pale aliposema
Katika Surat Baqarah, Aya ya 184 

"أياما معدودات "  Ni siku zenye kuhisabika"

- Na Allah ametufurashia funga hii ktk mwezi wa Ramadhani tu na kutusaameh ktk miezi 11 iliyobakia.

- Na wengine akawatowa katika hukmu ya faradhi; Kama vile msafiri, mgonjwa, mpumbavu, mwenye kupata hedhi na nifasi na wengineo pamoja kuwa wanalipa wengine na Kutowa fidya katika hao ,,

والله أعلم 

Read 3500 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba