Print this page

003: Nielezee funga za umma zilizopita; walikuwa wakifunga vipi❓

Written by

SWALI:

Sheikh :- Nielezee funga za umma zilizopita; walikuwa wakifunga vipi❓

JAWABU 

Naam ❗
Qur-an tukufu imethibitisha kuwa umma zilizotutangulia walikuwa wakifunga ... funga zao.. ..

Fungua Surat Baqarah. Aya 183

" ياأيها الذين ءامنوا كتب عليكم
الصيام كما كتب على الذين من قبلكم "

"Enyi mulioamini mumefaradhishiwa kufunga kama vile walivo faradhishiwa umma zilizotangulia "

- Namna na watu gani na idadi ndio tumetafautia na umma zilizopita na ktk hili kuna khilaafu baina maulamaa.

- Baadhi ya mapokezi yanasema kuwa mayahudi na manasara ndio waliofaradhishiwa kufunga, na mapokezi mengine yanasema ni umma zoote zilizopita.

- Walikuwa wakifunga siku 3 tu kwa mwezi na wa mwanzo kufunga Ramadhani ni Nabii Nuhi A. S.

Mapokezi mengine yanathibitisha kwamba kuwa manasaara walikuwa wakifunga Ramadhani lakini wakati wa juwa kali sana walikuwa hawaifungi Ramadhani bali walikuwa wakiichelewesha mpaka siku za usoni kisha huongeza siku 20 kwasababu ya kuchelewesha kwao huko .

- Na kabla kidogo ya kufaradhishwa funga hii ya Ramadhani ... Walikuwa wakifunga sunna tu sio funga ya faradhi.

- Na wako waliosema kuwa walikuwa wakifunga saumu nyengine ya fardhi kisha ikafutwa funga Yao hio kwa Kuja funga ya ramadhani .

Ufupisho

- Umma zilizopita walikuwa wakifunga kwa uthibitisho wa Qur-an .

- Idadi na jinsi walivokuwa wakifunga ndio kuna khilaafu baina ya maulamaa

 والله أعلم 

Read 2569 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba