Print this page

002: Nini maana ya saumu ( funga )❓

Written by

SWALI:

Sheikh,  Nini maana ya saumu ( funga )❓

JAWABU:

✏️ Saumu ni neno la kiarabu lenye harufu 3 za asili nazo ni ص/ و/م Saad/waaw/ mimu.

✏️ Neno hili kwa upande wa maana yake kilugha lina maana zifuatazo :--

1⃣- Kujizuiya na kitu na ukakiacha (kukinyamazia), yaani kunyamaza kimyaaa.

Allah anasema ktk Surat Maryam, Aya 26.  " إني نذرت للرحمن صوما"

Hakika yangu mimi nimeweka nadhiri kwa Rahmaan ( Allah) kuwa sitoongea ( na mtu yoyote yule).

2 -  Kutulia na kusimama; Kwa mfano unaweza kusema hivi , "صامت الريح"

Umetulia upeo na kunyamaza Au .. صام الفرس " Farasi Ametulia "

Hizi ni maana za kilungha yaani saumu ina maana ya ( kunyamaza, kujizuiya, kusimama.)

Ama neno hili kwa upande wa kisheria ni kujizuiya kila kina chofuturisha tangu kuchomoza kwa alfajiri ya kweli mpaka kuzama kwa juwa (loote) pamoja na kutia nia tangu usiku .

kujuzuiya na vinavo futurisha yaani kila vinavo haribu funga yako, kwa mfano maasi yoyote, kuywa au kula kwa maksudi, kuingiza kitu katika tundu zenye kufisha mpaka ndani , kufanya tendo la ndowa . Nk...

Unapaswa kujizuiya tangu adhana ya pili haijaadhiniwa mpaka juwa lizame lolote usiku hapo tena yafaa kula na kunywa na nk.....

Kutia nia tangu usiku ni sharti katika masharti ya funga sahihi bila ya kutia nia itakuwa funga yako baatili.

Kwa ufupi "funga imekuja ili itufunze uchamungu na kutupa afya na kuacha maasi maovu na kula na kunywa hata tendo la ndoa la halali.

 والله أعلم 

Read 5787 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba