Print this page

001: Nina suala "Nini maana ya Ramadhani" ❓

Written by

SWALI

Sheikh nina suala "Nini maana ya Ramadhani" ❓

JAWABU

✏️ Ramadhani (رمضان) ni neno la kiarabu latokana na neno la asli lenye harfu 3 za asili ( mujrrad), nalo ni ramadha (رمض) .

✏️ Neno ramadhani limetajwa ktk qur-ani surat baqarah aya 185 aliposema allah taalaa

"شهر رمضان الذي أنزل فيه القرءان "
Mwezi wa ramadhani ambao umeteremshwa ndani yake (ktk laylatu qadri) qur-an.

Na hakuna mwezi uliotajwa kwa jina lake ila mwezi huu kwa utukufu mkubwa uliopo ndani yake na fadhila zake.

wametofautiana maulamaa neno la (ramadhan) nini hassa maana yake, ufupisho wake ni kama hivi 

1⃣ - Amesema alkhalili kuwa maana yake ni mvua Huja kusafisha ktk ardhi na mavumbi.., yaani mwezi huu ukija husafisha miili ya binaadamu na maovu .

2⃣- na wako waliosema kuwA ramadha ni jiwe lilokuwa moto sanaa baada ya kupigwa na juwa kisawa sawa.

3⃣ - na wako waliosema kuwa ramadha ni unguzaji uliomkali .. Yaani kumainisha kuwa mwezi huu unaunguza madhambi ya waja wake Allah.

4⃣ - Amesema Mujaahid kuwa ramadha ni jina katika Majina yake Allah

Kwa ufupi ramadhani inamainisha kuwa kusafisha, kufuta, kuunguza, kutoharisha kila kichafu kiovu ktk mwili na roho

 والله أعلم. 

Read 6490 times
Said Al Habsy

https://www.ibadhi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Latest from Said Al Habsy

FaLang translation system by Faboba