Mkate wa kifaransa
- Written by Um Thuraiya
- Published in MAPISHI
- Add new comment
Mkate Wa Kifaransa
VINAVYOHITAJIKA NA - VIPIMO VYAKE
1. UNGA GRAM 700
2. SUKARI VIJIKO CHA SUPU KIMOJA
3. MAZIWA KIKOMBE KIMOJA.
4. MAYAI MANNE (2 YA KUPAMBIA JUU YA MKATE)
5.CHUMVI KIJIKO KIMOJA
6.HAMIRA GRAM 40.
7. MAFUTA 1/2 KIKOMBE (SUNFLOWER OIL)
8. SIAGI GRAM 100 ( YA KUPAKIA KWENYE MKATE)
9. UFUTA KIASI - WA KUPAMBIA JUU YA MKATE.
JINSI YA KUCHANGANYA NA KUANZA KUPIKA.
1. Changanya vifuatavyo, maziwa ( Yawe moto kidogo), hamira na sukari, upe mda ili upate kuumuka.
2. Changanya na uponde vifuatanyo, Unga,Chumvi,Hamira, Mayai Na Mafuta, ponda vizuri mpaka unga ulainike sana.
3. Ukishamaliza kuponda fanya madonge nane ya duara halafu sukuma Kama chapati kila moja baada ya moja paka siagi, ukishapaka weka nyingine juu yake mpaka wamaliza zoote nane. Hakikisha zoote umezitia siagi kwa juu, ya mwisho hutii kwa ajili utasukuma tena duara kubwa.
4.Utakata sasa kama unakata croissant, ukishakata pande nane wazungusha kama croissant halafu waikata mara mbili waweka kwenye tray yako ya kuchomea .
Madonge manne wazungusha kama madonge ya chapati utayaweka katikati ili kupata design mbili.
5. Tia mayai juu ya mkate na ufuta wacha kama nusu saa ufunike uumuke.
6. Time ya kuupika - hakikisha moto wako ni juu na chini, tazamia mara kwa mara ili kuhakikisha umeiva vizuri.
MZURI KWA BREAKFAST NA DINNER.