Biskuti Za Tende
- Written by Um Thuraiya
- Published in MAPISHI
- Add new comment
VINAVYOHITAJIKA NA - VIPIMO VYAKE.
1. UNGA VIKOMBE 2
2. SUKARI VIJIKO 2 VYA SUPU
3. SIAGI 200GRAM
5. MAZIWA VIJIKO 2 VYA SUPU.
6. VANNILA KIJIKO 1 CHA CHAI
7. BAKING POWDER KIJIKO 1 CHA CHAI
8. MAYAI MOJA
9. TENDE KIASI BILA YA TUMBA
10. ULEZI KIASI
JINSI YA KUCHANGANYA
Kuchukua siagi yako iliyokuwa laini uchanganye na maziwa na sukari huku unachanganganya unaweka vannila na baking powder,mwisho unaanza kutia unga pole pole mpaka wamaliza unga woote - unachanganya na mkono.
Ukiwa tayari unachukua tray ya kuchomea unatandaza unga wa biskuti chini halafu katikati wafanya mnyororo wa tende halafu waziba kwa juu na mchanganyiko wa biskuti wafanya mstari mrefu mpaka mwisho wa tray ukimaliza mistari yoote watia yai njano kwa juu na wanyunyizia ulezi halafu wazikata kama mkato wa kashata upande kidogo.
Baada ya hapo wazitia kwenye oven kwa moto wa 175 degree zikiwa tayari zitoe .
NZURI KWA KAHAWA