Chocobon
- Written by Um Thuraiya
- Published in MAPISHI
- Add new comment
VINAVYOHITAJIKA NA - VIPIMO VYAKE.
1. UNGA VIKOMBE 4
2. SUKARI VIJIKO 2 VYA SUPU
3. MAYAI MOJA
4. SIAGI 75 GRAM
5. MAZIWA KIKOMBE 1 CHA MUG.
6. MAJI 1/2 KIKOMBE.
7. CHUMVI 1/4 KIJIKO CHA CHAI.
8. HAMIRA KIJIKO KIMOJA KIKUBWA CHA SUPU.
9. VANNILA KIJIKO 1 CHA CHAI
10. MDALASINI VIJIKO 3 VYA SUPU.
11. MAZIWA MATAMU (CONDENSED MILK) KOPO MOJA DOGO.
12. KOROSHO (ZITWANGWE) KIASI.
13. MDALASINI VIJIKO 3 VYA SUPU.
14. SAUCE YA KUPAMBIA
JINSI YA KUCHANGANYA
Changanya vitu vyoote vya maji kwenye mashine anza kutia unga huku unasaga lakini Mdalasini na sukari usitie wakati wa Kuponda. Unga ukishaumuka sukuma upakie siagi kwa juu halafu chukua ile sukari na mdalasini uichanganye unyunyize kwa juu ya siagi. Ukishamaliza zungurusha kama roll ukate ndogo ndogo na kisu. Zipange kwenye tray zichome kwa moto wa 175 degree zikiwa tayari zitie maziwa matamu na zirushie vipande vya korosho
NZURI KWA KAHAWA