Buns Za Sukari
- Written by Um Thuraiya
- Published in MAPISHI
- Add new comment
VINAVYOHITAJIKA NA VIPIMO VYAKE.
1. UNGA VIKOMBE 3
2. SUKARI VIJIKO 4 VYA SUPU
3. MAYAI MAWILI
4. SIAGI 100 GRAM
5. MAZIWA KIKOMBE 1 CHA MUG.
6. HAMIRA KIJIKO 1 CHA SUPU
JINSI YA KUANZA KUCHANGANYA NA KUANZA KUPIKA
JINSI YA KUPONDA
Chukua maziwa, changanya na siagi weka kwnye moto mpaka iyayuke, ikashayayuka toa kwenye moto halafu ikishapoa weka hamira ndani ya maziwa,mayai ,sukari na chumvi weka kwenye mashine ya kusagia uanze kuweka unga kwenye mashine pole pole huku unasaga.
Ukishamaliza utoe unga woote ufanyie brush na mafuta halafu ufunuke uumuke. Ukishaumuka mda wa nusu saa aanza kufanya madonge ya duara madogo dogo uyatie kwenye tray ,chini ya tray pakaza mafuta kidogo ili unga usije ukashika au kunata katika hiyo tray, ukimaliza yafunike kama dakika 15 yakiumuka chukua yai la njano pakia juu ya mikate yoote, itakuwa tayari kwa kuchoma.
MIZURI KWA CHAI YA MAZIWA