Ibadhi.com

KUINGIA WATU WA OMAN KATIKA UISLAM KWA KHIYARI

Na ili ikamilike ile sura njema ing’aayo ya maibadhi, -ni vizuri kuelezea historia ya kuingia uislamu Oman ambao wengi wao ni Maibadhi-, hakika watu wa oman waliingia katika uislam kwa hiyari yao pamoja na viongozi wao Abd na Jeyfar watoto wa Julandaa Almaawali wanaotokana na Maawala bin Shams, Kisha ukasimama Uimam wa mwanzo kwa njia ya ukhalifa ulioongoka,dola yao  ikiongozwa na Imam Aljulanda bin Masoud Almaawali, kisha wakafuatana maimam kwa mfuatano unaofikia miaka elfu moja mpaka miaka ya hivi karibuni. Vile vile Maibadhi walisimamisha Uimam wa uongofu Yemen “Dola ya Talibul haq”, pia Aljeria kulikuwa na dola kubwa yenye maendeleo nayo ni ‘DOLA YA RUSTUMIYYAH”, Yote hayo kwa kufuata Njia iliyotakiwa na Allah mtukufu iliyo wazi katika kuendesha Hukmu, Njia iliyonyooka katika Qur an na sunnah. Na haya hutoyakuta kwa wengine, soma ukipenda yale aliyoyaandika Daktari wa  Ki imarati Hussein Ubeid Ghaanim Ghabbashi kuhusu Uimam na Demokrasia ya haki ambavyo vilisimamishwa na Maibadhi katika kitabu chake alichokiita “Omaan waddimuqratiyyah Al islaamiyyah” (Oman na demokrasi ya kiislam), Amesema: “Hakika harakati za kiibadhi zilipata muweko wake wa kiitikadi na kifikra mapema kabisa. Na kupitia kuhifadhi kwake misingi ya Shura, na uchaguzi huru wa maimamu, na msingi wa kukubaliana na kufunga baia’ (kiapo cha utiifu), yawezekana (madhehebu ya ibadhi) ikahesabiwa na ikajihesabu yenyewe kuwa ndio mrithi wa hakika wa nidhamu ya makhulafaa waongofu hasa kipindi cha mwanzo cha ukhalifa huo, zama za Abu bakr na Umar – Allah mtukufu awaridhie –


Kila sifa njema ni za Allah  mtukufu, Hakika katika madhehebu ya Ibadhi, tangu kuanza kwake mpaka sasa hivi inao wanachuoni wakubwa, hawa waliopo sasa wamepokea ilmu kutoka kwa waliopita kwa mfuatano kama dhahabu, ambao haukukatika kwa karne zote mpaka kufikia zama za masahaba watukufu kutoka kwa Mtume –Sallallahu alayhi wasallam- – kutoka kwa Jibriil – alayhi Salaam– kutoka kwa mola wetu mtukufu.
Na maktaba ya kiibadhi imejaa vitabu katika misingi ya dini na matawi yake, baadhi ya utungaji wao unapita juzuu tisini, bali unaweza kumkuta mwanachuoni mmoja na utungaji wa zaidi ya vitabu mia tatu mfano : Qutbul Aimmah (Kiongozi wa Maima) Sheikh Muhammad bin Yousuuf Atfeish –Allah mtukufu amridhie-, vitabu vilivyochapishwa mpaka sasa ni sehemu ndogo kuliko vile ambavyo havijachapishwa !!, kwa hivyo mwenye kutaka uhakika arejee katika vitabu vya madhehebu yetu, sio asikie au asome katika vitabu visivyokuwa vyao ili abainikiwe na uhakika wa wazi, ambao atashikamana nao na ataitakidi uhakika huo kwa idhini ya Allah mtukufu.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment