Ibadhi.com

SALAM MOJA NDIO MASHUHURI KATIKA MADHEHEBU

SALAM MOJA NDIO MASHUHURI KATIKA MADHEHEBU

Amma jambo la kutoa salam wakati wa kumaliza sala amesema kuhusu hilo Al-imam Assalimiy:

Toa salam kulia na kushoto *** salam mbili, na iliyo mashuhuri ni moja

Kwa hivyo riwaya ya salam moja ndio mashuhuri kwa Maibadhi pamoja na kujuzu kwa salam mbili, na dalili ya salam moja ni kile alichokipokea Mama wa waumini Aisha na Salama bin Al ak-wa’a na Sahl bin Saad – Allah mtukufu awaridhie- kwa Tirmidhi na Ibn Majah na Ahmad “Hakika Mtume s.a.w. alikuwa akitoa salam moja, na walikuwa muhaajiriina wanatoa salam moja, na kwa ajili hiyo Amesema Al imam Annawawi Mshafi “Wamekubaliana wanachuoni ambao ni wenye kuzingatiwa kuwa hakika si wajibu katika sala ispokuwa salam moja tu” na Amesema Ibnul Mundhir “Na wamekubaliana – wanachuoni – kuwa inajuzu sala ya atakayeishia kwa salam moja tu”


Ndugu yangu Muislam hakika kufuata kilichothibiti na kilichokubalina ndio bora  na salama zaidi kwa dini yako na sala yako ambayo ni jambo la kwanza atakalokuuliza mola wako siku ya Qiyama “Na wenye kuhakikisha mambo katika wanachuoni pamoja na tofauti ya madhehebu zao hawaikubali hadithi Aahaadi kuwa ni hoja katika masuala ya kiitikadi, kwa kuwa haifidishi yaqini, na kwa ajili hiyo imekuwa sala ambayo ipo jirani na itikadi ichukuliwe kwa tahadhari. Kama ambavyo wapo katika wanachuoni waliosema sala ya kiibadhi Imethibiti kwa Ijmaa kwa kuwa wanayoyaacha katika matendo ya sala, wengine wametofautiana katika kuthibiti kwake”

 

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment