Ibadhi.com

TATIZO LA WINGI NA NAMNA

TATIZO LA WINGI NA NAMNA


Jua – ewe ndugu yangu mpenzi – kuwa HAKI NI HAKI hata kama wafuasi wake ni wachache, mazingatio ni namna mlivyo sio wingi. Hakika Mtume –Sallallahu alayhi wasallam- akiwa na masahaba wake katika vita ukipima kwa idadi na washirikina, nani walikuwa wengi? Leo hii waislam ni wangapi ukilinganisha na makafiri.? Na wangapi leo wanasali alfajiri kwa jamaa ukiinganisha na waliolala, na ujue kuwa walio bora, wenye kufanya vizuri, na wakawa juu huwa ni wachache ukilinganisha na wengine.
Hakika Allah mtukufu hakusifu wingi katika kitabu chake kitukufu, ispokuwa amesema:

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ - يوسف: ١٠٣

“Na watu wengi  hata kama utajitahidi si waumini” Yusuf:103

Na amesema pia:

وَإِنْ تُطِعْ أَكْثَرَ مَنْ فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ ۚ 

“Na kama utawatii wengi katika walio ardhi, watakakupoteza kunako njia ya Allah mtukufu” An aam:116

“Lakini wengi katika watu hawajui” Yuosuf : 21, Nahl:38, Ruum:3, Sabaa:28,36, Ghaafir:57, Jaathiyah:26.

وَقَلِيلٌ مِنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ

“Ni makundi machache mangapi, yamewashinda makundi ya watu wengi kwa idhni ya Allah mtukufu” Baqarah:249

 كَمْ مِنْ فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّهِ

 

Basi thibiti katika msimamo wako ewe ndugu yangu na eneza uongofu ambao unao, hakika wewe upo katika haki ya wazi.

 

 

 

 

 

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment