Ibadhi.com

MAHUSIANO NA WENGINE

MAHUSIANO NA WENGINE


Katika mahusiano na wengine Inazingatiwa madhehebu ya Ibadhi ni katika madhehebu bora kuliko madhehebu  zingine, hayo yamethibiti zamani na sasa, kwa sababu ya ufaham wao wa juu wa maelekezo ya Allah mtukufu  yaliyokuja yakisema : “Hakika ummah wenu huu ni ummah mmoja, na mimi ndio mola wenu nicheni” Muuminiin:52 hilo limepekea lengo lake kuwa wazi, na lengo lao ni kupenda kwao kikweli kweli kuifikia HAKI,  kutoka kwa yoyote atakayekuja nayo, vitabu vyao na athari zao vinashuhudia haya, na katika mifano ya wema waliotangulia Qauli ya Abii Hamza Alshari Alsuleimy – Allah mtukufu amrehem- naye akiwa juu ya mimbar ya Mtume s.a.w. katika mji wa Madina aliposema: “Watu wote ni katka sisi na sisi ni katika wao ispokuwa watu namna tatu: Mwenye kumshirikisha Allah mtukufu, mwenye kuabudu mizimu, au Kafiri katika waliopewa kitabu, au kiongozi muovu aliyejiweka katika utawala juu ya waja wa Allah kwa kuhukumu tofauti na alivyoteremsha Allah mtukufu”{9}

Na katika misimamo ya wanachuoni wa zama za mwishoni ni Qauli ya Imaam Saalimi – Allah amrehemu –


وَنَحْنُ لَا نُطَالِبُ العِبَادَ *** فَوْقَ شَهَادَتَيْهِمُ اعْتِقَادَا
فَمَنْ أَتَى بِالْجُمْلَتَيْنِ قُمْنَا *** إِخْوَانُنَا وَبِالْحُقُوْقِ قُمْنَا


Waibadhi hatutaki  *** ispokuwa kwa haki
Shahada mbili hakiki *** kwa ndugu zetu sikia
Ukisemea mashariki *** ni ndugu yetu rafiki,
Haki zote stahiki *** kwetu sisi takutia


Vile vile dola walizosimamisha Oman, Tehart na Yemen zinashuhudia heshima yao na uzuri wa mahusiano yao na wengine, kwani ilikuwa kuishi kwa amani, kuheshimu itikadi na madhehebu nyingine ndio alama za Ibadhi.
Anasema mwanachuoni mmisri Aliyekufa Shahid, Sayyid Qutb “Kwa bahati nzuri sana, Fiqh ya madh-hab ya Ibadhi na misingi wanayoisimamia ina usawa unaoruhusu kukutana na wengine kwa yale ambayo muislam anakuwa ni muislam katika asili ya dini na misingi yake ya mwanzo – kwa mujibu wa tujuavyo -, na hayo yanatosha”{10}

 

----------------------------------------------------------------------------------------

{9} Tabari: Taarikhul umam wal muluuk jz 4 uk 329, Ally bin Hussein Al isfahaani: Al aghaani jz 2 uk 104, Ibn Abd Rabbih Al andalusi: Al aqdu alfariid jz 4 uk 144- 1147, Ahmad Zaki Swafuut: Jamharat Khutabu l arab fil usuuri al arabiyya Azzaahirah jz 2 uk 477

{10} {10} Majallat Shiha Almisriyya, Idadi 15, Jumadal uula 1367h/March 1948m

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment