Ibadhi.com

KUPAMBANUKA

Kwa kuwa Ahlu naharawaan ((Almuhakkima)), wakiwemo masahaba baina yao, walikuwa ni wenye kukataa amri ya TAHKIIM,[6] wakajitenga mbali na fitna na wakatoka kwenda katika sehem iitwao Nahrawaan. Na ilikuwa Njia yao ni kutotumia nguvu, na kutohalalisha damu na mali za wapinzani wao LAKINI kwa muda mfupi Naafi bin Azraq na kundi lake la Azaariqah, pia kundi la Najdaat, pia kundi la Sufriyya, walipwekeka na hukmu ya peke yao, ilojengeka juu ya msingi wa kuwakafirisha wenye kuwakhalifu na wenye madhambi makubwa[7]  na kuzihalalisha damu zao – kuwauwa—na kwa ajili hiyo wakawa wao na wote waliowafuata katika fikra hiyo ya kukafirisha na kuua, ni miongoni mwa MAKHAWAARIJI.
Tofauti na Ibadhi, kwani wao hawakuwafikiana na rai yao na kwa ajili hiyo yalitokea mapigano baina ya Sufriyya wakiongozwa na Shaiban Mkhawaarij walipotaka kuingia Oman, Ibadhi wakampiga vita huyo Shaiban, kwa uongozi wa Imaam Aljulanda bin Massoud – Allah amrehem -, Walhamdulillah hakuna Khawaariji waliobaki ispokuwa baadhi ya wale waliobeba fikra zao katika kuua, kuripua mabomu, na kuwakafirisha wasilamu, kwa sababu ya ususuavu wa kimadhehebu au kwa hoja ya Jihad.!!


نَـجَوْنَا بِـحَمْدِ اللهِ مِنْهَا عَلَى هُدًى *** فَنَحْنُ عَلَى سَيْرِ النَّبِيِّ نَسِيْرُ  


Ni za mola sifa  njema,  tumeokoka mapema, fitina tumeihama, twamfuata Nabiya.

--------------------------------------------------------

[6] - TAHKIIM: tukio la kuwahukumisha watu kaika hukmu ambayo tayari Allah ameshaitoa, pale Muawiya alipokaribia kushindwa akaja na hila ya kunyanyua misahafu, ilopelekea Abu Musa Al ash’ary na Amru bin Al aas kuhukumu kinyume na hukmu ya Allah mtukufu katika suurat alhujurrat:9, na akauzuliwa uongozi Ally bin Abii Talib. K.W. ( Mtarjimu)

[7] - Ukafiri wa kishirkina. ( Mtarjimu)

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment