Ibadhi.com

MIZIZI YA KIHISTORIA YA MADHEHEBU HII

MIZIZI YA KIHISTORIA YA MADHEHEBU HII

Dola ya Umayyad ndiyo iliyowapa Ahlul haqq wal istiqama jina la Ibadhi, kwa kuwanasibisha na Abdullah bin Ibadh Altamimi R.A., kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mtetezi wao, na mwenye kuweka wazi  fikra zao, wakaridhia Ahlulhaq wal istiqama kuitwa huko, LAKINI muasisi wa uhakika wa chuo hichi cha Ibadhi ni Mfuasi mkubwa wa mwanzo mwanzo wa masahaba Imam  Jabir bin Zaid –Allah awe radhi naye- aliyekufa mwaka 93h, ambaye alijifundisha na kuchukua elimu kutoka kwa Sayyida Aisha, Ibn Abbas, Ibn Umar na wengineo katika wakubwa wa masahaba – Allah awe radhi nao –jambo lilopelekea kunyanyuka juu kwa cheo chake cha kielimu hata kufikia Ibn Abbas kusema “Muulizeni Jabir bin Zaid, kwani lau wangemuuliza watu wa mashariki na magharibi ingeliwatosha elimu yake”[3] na baada ya kufariki kwake alisema sahaba mtukufu Anas bin Malik – Allah awe radhi naye – “ Leo amefariki aliyekuwa mjuzi zaidi juu ya ardhi”[4] na hivyo ikawa  manhaj ya Imam Jabir bin Zaid R.A. katika kuyawekea dalili  mas-ala ya kielim na kutoa hukmu ndani yake ndio njia ya Ibadhi mpaka leo.

Na kwa ajili hii inahesabiwa madhehebu ya Ibadhi ndio madhehebu ya mwanzo na iliyo kongwe zaidi, bali ni madhehebu ya masahaba – Allah awe radhi nao – kwani amezaliwa Imaam Jabir bin Zaid mwaka 18h, hali ya kuwa amezaliwa Imaam Zaid bin Ally mwaka 79h,[5] na Amezaliwa Imaam Abu Hanifa mwenye madhehebu ya kwanza katika madhehebu za kisunni mwaka 80h
Na ilipoanza kukua  madrasa ya Kiibadhi (( Ahlul haqq wal istiqaama )), walijiunga Ahlu nahrawaan, wale waliokuwa na kundi la Ally K.W. katika vita dhidi ya Muawiya na jeshi lake la uasi, na kwa hakika Ahlu nahrawaan walifikia kuleta natija iliyokuwa bora zaidi na nzuri yao walipomnasihi Ally bin Abi Talib – Imaam na khalifa wa kisheria – kuendelea kulipiga kundi la waasi mpaka lirejee katika haki na kuwa chini ya kiongozi wa waumini ((Khalifa Ally bin Abi Talib)), Amesema Allah mtukufu : “Ikiwa kundi moja litaasi dhidi ya mwingine basi lipigeni lile liloasi mpaka lirejee katika amri ya Allah mtukufu Hujuraat:9
Lakini Ally – K.W. – Aliwacha kupigana, ukadhoofika utawala wake na udhibiti wake wa dola, na ikawa miji ya Sham ni katika milki ya Muawiya.

------------------------------------------------------------------------

[3] - Addurjeiny,Al tabaqaat jz 2 uk 205. Alshammakhi, Alsiyar jz 1 uk 67. Alharthi Alumaaniy, Aluquud aalfiddhiyyah uk 95. Ahmed bin Soud Alsiyabi, Alraf’u waldwammu fii salaat uk 10

[4] - Alshammakhi; Alsiyar jz 1 uk 68, 

[5] - Zaid bin Ally Imam wa madhehebu ya Zaidiyya katika madhehebu za kishia. Naye ni wa mwanzo katika maimam wa madhehebu za kishia, wa pili katika wao ni Jafar Alsaddiq imam wa Shia Imaamiyya aliyezaliwa mwaka wa 80h. (mtarjimu)

%MCEPASTEBIN%
Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment